WAKILI AJITOSA KUGOMBEA UBUNGE KALAMBO




Na Peti Siame,Rukwa

WAKILI,Fortunatus Mpangamila Sichone (45) ametangaza rasmi nia ya kugombea ubunge jimbo la Kalambo lililopo mkoani Rukwa katika uchaguzi Mkuu ujao kupitia CCM.

Mbunge wa Jimbo hilo ni Josephat Kandege.

Sichone ambaye ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Mkoa kupitia Jumuiya ya Wazazi ,akizungumza na HabariLEO alisema kuwa ameamua kugombea ubunge jimbo la Kalambo baada ya kuona hali ya maendeleo ya jimbo hilo ikiwa siyo nzuri kwa miongo kadhaa.

" Nimekuwa na ndoto ya kuwakilisha wananchi bungeni tangu nikiwa mtoto miaka 30 iliyopita .... Jimbo la Kalambo lina changamoto kadhaa kubwa ni migogoro ya ardhi imekuwepo tangu nikiwa mdogo hadi sasa " anasisitiza.



Aliongeza kuwa wakati ukifika atachukua na kujaza fomu za kugombea ubunge katika Jimbo la Kalambo akisisitiza kuwa atatumia taaluma yake ya Sheria kusaidia kusuluhisha migogoro ya ardhi inayowakabili wananchi wa Jimbo hilo kwa miaka mingi.

Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa