KATIBU MKUU UMOJA WA SHULE ZA SEKONDARI NCHINI ACHUKUA FOMU YA UBUNGE.





''Kugombea ni haki ya kila mtanzania,hivyo nimetia nia ya ubunge kuomba ridhaa kwa chama,nina malengo makubwa ya kuipaisha Mbozi kiuchumi,kuweka mikakati endelevu kwenye zao la Kahawa''

Na Ibrahim Yassin, Songwe

Katibu mkuu wa Umoja wa wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania Bara na kada lia lia wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Frank Ndile amechukua fomu ya kuomba kuteuliwa na Chama hicho kugombea nafasi ya ubunge Jimbo la Mbozi Mkoani Songwe.

Ndile leo June 29,2025 amefika katika ofisi za chama hicho zilizopo wilaya ni Mbozi Mji wa Vwawa mkoani hapa na kukabidhiwa fomu na katibu wa chama hicho wilaya ya Mbozi Julius Mbwiga.

Ndile ambaye pia ni meneja wa shule za sekondari Kanan amesema amewiwa kuchukua fomu kugombea ubunge Jimbo la Mbozi kwa lengo la kuwatumikia wananchi ikiwepo kutatua chagamoto zilizopo.

katibu wa ccm wilayani Mbozi yenye majimbo mawili Julius Mbwaga akimkabidhi fomu ya kugombea Frank Ndile aliyevaa kofia.katika ofisi za ccm wilayani humo.
Alizitaja changamoto mbalimbali ikiwemo kuboresha  miundombinu ya barabara ili kurahisish usafirishaji wa mazao yanayotikana na kilimo ambacho wananchi wake ndiyo kiinua mgongo chao.

Aliongeza kuwa zao kuu la biashara wilayani Mbozi ni zao la Kahawa hivyo ili wakulima wanufaike wanatakiwa watengenezewe miundombinu rafiki ya barabara,maji,soko la uhakika na utoaji wa elimu kwa vijana ili wavutiwe kulima zao hilo.

''Mimi ni mzaliwa wa wilaya hii ninafahamu changamoto zilizopo,nikipewa ridhaa ya kuwa mbunge wananchi hawatajuta,nitahakikisha ninagusa kila sekta muhimu ili wananchi wainuke kiuchumi''amesema Ndile.

Hata hivyo Ndile mbali na kueleza mikakati yake ya kuwatumikia wananch i,alimpongeza Rais Dkt,Samia Suluhu kwa kujenga miradi midogo na miku bwa inayogusa jamii akiamini kuwa awamu ijayo ataing'arisha zaidi Nchi.

''Ndugu wanahabari,Rais Samia ni mmoja wa marais aliyeingia kwenye historia kubwa duniani kwa uchapaji kazi wake na kuifanya Tanzania kuwa ni ya mfano Afrika kwa jinsi ilivyo na maendeleo''amesema Ndile.



Kasi ya watia nia katika jimbo la Mbozi na Vwawa inazidi kuongezekwa kwani kwa siku mbili pekee jimbo la mbozi watia nia zaidi ya 10 wamechu kua fomu huku jimbo la Vwawa wakifikia zaidi ya 8,idadi kamili itapatikana baada ya chama kukamilisha mchakato.

Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa