MADAKTARI BINGWA WAPOKELEWA NKASI KWA BASHASHA


Na Israel Mwaisaka,Nkasi
WANANCHI wilayani Nkasi Mkoani Rukwa wamewapokea Madaktari bingwa Kwa bashasha Huku wakihaidi kuwapatia ushirikiano wa kutosha katika kipindi chote watakachokuwepo wilayani humo.
Akizungumza wakati wa mapokezi ya Madaktari hao Kaimu Mganga mkuu wa wilaya Josepha Joseph amesema kuwa ujio wa Madaktari .hao ni utekelezaji wa programme ya Rais jamuhuri ya muungano wa Tanzania DK,Samia Suluhu Hassan hivyo ni muhimu Kwa Wananchi hao kuitumia fursa hiyo vizuri.
Amesema kuwa Madaktari hao watano watakuwepo wilayani Nkasi Kwa muda wa siku Tano na wapo watano wakiwa wamebobea katika nyanja mbalimbali kama Vile katika magonjwa ya Kina Mama na Wajawazito,magonjwa ya Watoto,upasuaji,usingizi na magonjwa ya ndani kama Presha na kisukari.
Kaimu mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya Ladislaus Mzelela Kwa upande wake amewataka Wananchi wote kuhakikisha watu wote wenye shida za kiafya kuitumia vizuri fursa hiyo na kuahidi wa kama halmashauri kuwapatia ushirikiano wa hari na Mali Wataalamu hao pale itakapohitajika Ili shughuli hiyo isiweze kukwama.
Amedai kuwa huduma hizi za kibingwa ni ngumu Saba kuzipata na hata zikipatikana upatikana Kwa gharama kubwa hivyo ni muhimu sana kwao kuona Mpango huo unafanikiwa Kwa kiasi kikubwa na lengo la serikali ni kutaka kuona Watu wake wanakua na afya Bora.
Pia aliitumia fursa hiyo kumpongeza Mhe,Rais DK,Samia Suluhu Hassan Kwa kuanzisha Mpango huo wa kuwapeleka Madaktari bingwa Hadi vijijini na kuwa jambo Hilo ni kubwa na ni lazima usimamiwe na kuhakikisha unakua na tija.


Wakizungumza baada ya mapokezi hayo baadhi ya Wananchi waliojitokeza kwenye mapokezi hayo wamedai kwamba wait wamefurahishwa na ujio wa Madaktari hao bingwa na kuwa wamekua na uhitaji wa huduma za afya za kibingwa na kuwa sasa zimewafikia Hadi nyumbani.
Wamesema kuwa watajitahidi kuhakikisha wale wote wenye uhitaji wa huduma hizo za kibingwa wanazifikia Kwa lengo la kuimarisha afya kama lilivyo lengo la Mhe,Rais Samia Suluhu Hassan




Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa