RUWASA YATAKIWA KUVILINDA VYANZO VYA MAJI
Na Israel Mwaisaka,Nkasi
MKUU wa wilaya Nkasi Peter Lijualikali amewaagiza Wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini RUWASA kuhakikisha wanavilinda vyanzo vya maji kwa kuzuia watu kulima karibu na vyanzo vya maji ikiwa ni pamoja na kupanda miti ili kulinda hifadhi hizo
Maagizo hayo ameyatoa leo alipokuwa akitembelea na kukagua miradi ya maji ambapo ameweza kutembelea mradi wa maji Kabwe, Matala,Kirando na Mkinga ambapo amesema kuwa vyanzo vyote vya maji inabidi vilindwe ipasavyo na kuhakikisha shughuli mbalimbali za kibindamu zinafanywa mbali na vyanzo hivyo.
Amesema kuwa ili miradi hiyo iweze kudumu na kuleta tija kwa jamii ni lazima itunzwe kisheria ili jamii iweze kupata maji wakati wote na kuondoa tatizo la maji katika jamii kama ilivyo ndoto yam he,Rais ya kumtua ndoo Mama kichwani .
Akitoa taarifa kwa mkuu wa wilaya kaimu meneja wa RUWASA wilayani Nkasi Jaffari Amri amesema kuwa miradi mitatu ya maji ya Kabwe,Kirando na Mkinga imepata changamoto baada ya maji ya ziwa Tanganyika kuvamia vyanzo vyake vya maji
Akitoa taarifa kwa mkuu wa wilaya kaimu meneja wa Ruwasa wilayani Nkasi Jaffari Amri amesema kuwa mradi wa maji Kabwe umepata changamoto baada ya maji ya ziwa Tanganyika kuvamia vyanzo vya maji na kupelekea mfumo wa kuendesha mitambo kuwa ndani ya maji na kushindwa kufanya kufanya kazi.
Mkuu wa wilaya kwa upande wake amemtaka katibu tawala wa wilaya kuhakikisha kuwa anamuandikia barua katibu mkuu mkuu wa wizara ya maji kumweleza uhalisia wa hari ya miradi hiyo ili kuona namna ya kupata fedha ili waweze kuihamisha mifumo ya mitambo kutoka kwenye maji ili iendelee kufanya kazi.
Amedai kuwa miradi hiyo kusimama kufanya kazi kunawatesa wananchi na ipo haja kwa serikali kulifanyia uharaka jambo hilo ili maji yaendelee kutoka ili kuywaondoa Wananchi kwenye janga la maradhi ya milipuko kwa kuendelea kutumia maji yasiyo salama



Comments
Post a Comment