JESHI LA POLISI LAKOSHWA NA USHIRIKIANO ULIOPO NA WANANANCHI



Na Ibrahim Yassin,Songwe

JESHI la polisi nchini limewapongeza wananchi wa mikoa mbalimbali nchini hasa ile iliyopo kwenye mipaka na nchi jirani ikiwemo mkoa wa Songwe kwa kuvuka mwaka kwa amani ukilinganisha na miaka ya nyuma.

Mkoa wa Songwe una wilaya mbili zinazopakana na nchi jirani ambazo ni Ileje inayopakana na nchi ya Malawi na halmashauti ya mji Tunduma inayopakana na nchi ya Zambia.

Akizungumza Januari 2 /2024 kwenye ukumbi wa jeshi hilo mkoani Songwe msemaji wa Jeshi la polisi nchini David Misime, alisema elimu inayoendelea kutolewa na jeshi la polisi kwa wananchi kupitia makundi mbalimbali kuhusu kuacha masuala ya uhatifu umesaidi kupunguza vutugu.



Alisema katika sherehe za mkesha wa kuvuka mwaka 2023 na kuukatibisha mwaka 2024 hakuna matukio ya uharifu,wizi,ubakaji na unyang’anyi wala watu kuumizana na kwamba hii inatokana na watu kuelewa madhata ya kufanya uhatifu.

‘’Ndugu wanahabari watu wamesherehekea sikuku ya mwaka mpya kwa amani,tunataka amani hii iendelee kuwa hivyo ndiyo maana tunazunguka nzi nzima na makamanda wa mikoa wanapita kwenye nyumba za Ibada,na kwenye mikusanyiko mengine kutoa elimu,’’alisema Misime.

Aidha Misime alisema zoezi hili litakuwa endelevu,kwani mbali na kuendesha zoezi hili,zipo changamoto mbalimbali ikiwemo baadhi ya watu wachache wnaoendesha matukio ya kuumizana kutokana na wivu wa mapenzi na kwamba bado elimu inaendelea kutolewa dhidi yao.

Pia amewataka wazazi kuwa na malezi bora kwa watoto na suala la marezi bora lipewe kipaumbele mashuleni ili watoto wawe na makuzi mazuri.

Alisema zoezi la kutoa elimu kwa jamii ni mikakati endelevu na hata Tume ya haki jinai imekuwa ikifanya kazi kubwa ya kuelimisha jamii kupunguza uhatifu na kuuzuia.
FM 

Suala hili la utoaji elimu limekuja wakati muhafaka kwa mkoa wa Songwe wenye matukio mengi ya kujeruhi kwa wivu wa mapenzi na kuuana kwani siku ya Disemba 11/2023 mzee Magao Msangawale (90) mkazi wa kijiji cha Hangomba Mbozi alikutwa ameuawa na watu wasiojulikana.

Na pia Disemba 12/2023 mkazi wa kijiji cha Hangomba Mbozi Aloyce Magao (34) aligundulika kuuawa na kufukiwa kwenye shimo mbugani na watu wasiofahamika kabla ya umauti wake alionekana Grocery na wenzake wakinywa vinywaji, hivyo elimu izidishwe kutolewa.

Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa