UWT watakiwa kujipanga na uchaguzi serikali za mitaa
Na Israel Mwaisaka,Nkasi
MBUNGE wa viti maalumu mkoa Rukwa Bupe Mwakang'ata (CCM) amewataka Wananchi kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la wakazi ambalo litatumika kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.
akizungumza kwenye kikao cha baraza la Wanawake (UWT) jana amesema kuwa zoezi la uandikishaji wakazi litaanza hivi karibuni hivyo litakapoanza ni vyema wakajitokeza kujiorodhesha kwani daftaro hilo ndilo litakalotumika kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.
amesema kuwa ili uweze kupata haki ya kushiriki kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na kuweza kuwachagua viongozi wawatakao ni lazima wajiorodheshe katika daftari hilo.
"Wanawake kama mnataka chama chetu kishinde kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa ni lazima sisi wenyewe tujitokeze kujiandikisha kwenye daftari hilo na tuwahamasishe na wenzetu kujitokeza kujiandikisha pindi zoezi litakapoanza" alisema
Na aliwataka Wajumbe wa baraza hilo la UWT kuendelea kupendana na kuepuka migawanyiko ndani ya chama na wasikubali kugawanywa na watu wenye roho za madaraka bila utaratibu.
Mwenyekiti wa UWT mkoa Rukwa Auleria Kanyengere kwa upande wake aliwahimiza Wanawake kupitia jumuia hiyo kuwahimiza Watoto wao kwenda shule hasa katika kipindi hiki ambacho shule zimefunguliwa kwani Watoto kupata elimu hiyo ni haki yao ya msingi.
amesema katika kipindi hiki ambacho Mhe,Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt,Samia Suluhu Hassan amejitahidi kujenga majengo mazuri kwa ajili ya madarasa hivyo ni vizuri tukaziunga mkono jitihada hizo nzuri za Rais kwa kuwapeleka Watoto shule.
Mwakang'ata pia alitumia fursa hiyo kugawa vifaa vya michezo kwa Watu wa makundi mbalimbali kama Bodaboda,Wanafunzi na wengine kuutumia muda wa ziada kufanya michezo.


Comments
Post a Comment