BIBI MJANE AMUANGUKIA RAIS DR,SAMIA KUPOKWA MALI ALIZOACHIWA NA MUMEWE IKIWEMO HEKARI 31 ZA ARDHI.

MAKALA

APANGA KWENDA IKULU KUONANA NA RAIS DR,SAMIA KUELEZA ANAVYONYANYASIKA JUU YA MALI ALIZOACHIWA NA MUMEWE


mjane Mariam Kalupande akizungumza na mwandishi wa habari jinsi ardhi yake inavyotaka kuporwa.
Na Israel Mwaisaka
WAKATI serikali ya awamu ya sita ikiongozwa na Rais Dr,Samia Suluhu Hassan ikiwaagiza viongozi ngazi zote kuhakikisha inamaliza migogoro ya ardhi nchini,hali hiyo imekuwa tofauti kwa wilaya ya Mbozi mkoani Songwe ambako bibi mjane ananyanyasika juu ardhi zake.

Ardhi inathamani kubwa katika kuendeleza maisha ya binadamu ambayo inatumika kwa kujenga nyu mba za biashara ,viwanda,Taasisi ,makazi na kuendesha shughuli za kilimo kwa mazao ya biashara na chakula hivyo endapo inatokea migogoro inaweza  kuzuka mapigano na kuhatarisha uhai wa watu.

Hali hiyo imeikumba familia ya mzee Leston Kalupande aliyeanzisha taasisi ya kusaidia jamii ambaye kwa sasa ni marehemu ,baada ya kifo chake kumezuaka mgogoro mzito ambapo mdogo wake anadaiwa kunyang’anya mali za taasisi na sasa yupo kwenye mikakati ya kupoka ardhi.

Akisimulia mkasa huo,kaka wa marehemu Kalupande Jipson Mwayela anasema  mwaka 1985 babu yake Shangala Halinga jina la utoto aliitwa Mwile Msobhanjele alimpatia eneo  Kalupande na mwaka 1989 alianza kujenga msingi na 1991 kulikuwa na nyumba 2  na sasa zipo 5 yeye  akiwa msimamizi.

Anasema yeye aliendelea kusimamia ujenzi wakati Kalupande yupo Morogoro akisimamia kiwanda cha kutengeneza Maturubai na ilipofika mwaka 1991 akarejea nyumbani na kuifuata serikali ya kijiji akihitaji hati miliki za viwanja na ndipo alipoanzisha Taasisi.

Amesema  baada ya kumaliza ujenzi alianza kazi ya kuiendesha taasisi hiyo iitwayo,Wakina mama na watoto Foundation (Self Development Program) huku yeye pamoja na mtoto wa dada yake,Rozina Kalupande aliyemlea na kumsomesha waliingizwa kwenye bodi.

Mzee Mwayela  anaendelea kusema kuwa marehemu Leston Kalupande alikuwa ndiye kiongozi muasisi wa Taasisi hiyo,akishirikiana na rafiki yake Karin Vetter  mzungu raia wa Uswisi aliyekuwa ni mmoja wa wafadhiri waliofanya kazi kwa ushirikiano mkubwa.

Treka na gari Toyota na vifaa vingene vilivyohamishwa kinyemela kutoka eneo kuu la ofisi na kupelekwa eneo lingine.

Anasema katika utendaji  uliotukuka waliweza kusafiri pamoja hadi Uswisi na kufanikiwa kutafuta fedha ambazo zilitumika kwenye kazi mbalimbali za maendeleo ya kijiji cha Hezya na Haraka ikiwemo kujenga miradi ya maji,vyumba vya madarasa ,Vyoo pamoja na daraja katika maeneo korofi.

Anasema ilipofika terehe 17/9/2012 mzee Leston Kalupande alifariki dunia hivyo kazi zote zilikuwa chini ya Mzungu  Karin na hakukuwa na shida,ilipofika Disemba 7/2014 Mzungu Karin alipofariki na kuzikwa eneo moja na rafiki yake Kalupande huku ndugu kutoka Uswisi  wakishiriki maziko hayo Mbozi Tanzania.

Anasema baada ya waasisi hao kufariki,alipatikana mzgungu mungine raia wa Uswisi kuifadhiri taasisi hiyo,ndipo dada huyo wa marehemu alipoanza fujo akinyang’anya mali ambazo ni Matrekta mawili,na vifaa vingine na kuvihamisha eneo la taasisi na kupeleka eneo lingine.

Anasema baada ya kufanikiwa kupokonya mali hizo,na sasa anataka kupokonya ardhi yenye ekari 31 akibadirisha hati na ndipo kesi ilipofunguliwa mahakamani na mjane huyo kupata ushindi lakini wakati kesi ipo mahakamani alipata taarifa kuwa mazao aina ya Kahawa yalifyekwa huku watu 6 walifika kwa mjane na kumtishia.

‘’Mimi miaka ya nyuma niliwahi kuwa mwenyekiti wa kijiji hiki,nafahamu vyema hali ilivyo,huyu mare hemu ni mdogo wangu tumechangia mama alipokabidhiwa ardhi hii na babu nilikuwepo,nashangaa mtoto huyo amepata wapi ujasili wa kuisumbua familia iliyomlea na kumsomesha,’’anasema Mwayela.

Shuhuda mungine ni Lameck Ndabila anasema yeye alikuwa mwenyekiti wa kijiji hicho cha Haraka mwaka 2014 hadi 2019 wakati marehemu Kalupande anaomba hati alikuwepo na eneo hilo ni lake na mgogoro uliibuka mwaka 2017 kipindi cha madai ya hati.

Anasema baada ya Kalupande kuomba hati miliki ya eneo lake,wajumbe wa serikali ya kijiji chini ya afisa mtendaji  walikaa na kuamua kumpatia hati ambayo ilikuja kupokonywa na mkuu wa wilaya wakati huo John Palingo aliyedai eneo ni  la WAKINA bila kujua Taasisi ilikuja wakati ardhi ipo.

‘’Ndugu Mwandishi,eneo alipewa marehemu Kalupande na babu yake,Taasisi ya WAKINA iliasisiwa na Kalupande unapozungumza taasisi ya WAKINA unamzungumzia Kalupande,sasa alishangazwa na kitendo kilichofanyika lakini Mjane alipoenda mahakamani ameshinda kesi lakini bado ananyanyasika.

Shari Kalupande  ni mtoto wa marehemu ,anasema mali zilizopo ikiwemo ardhi ni mali ya baba na alipofariki imebaki kuwa mali ya famillia mama ndiye msimamizi mkuu,anashangaa kuona shangazi Rovina kuwa na tamaa ya mali na kuisaliti familia iliyomlea na kumsomesha.

‘’Ndugu mwandishi huyo ni shangazi yangu amelelewa katika familia hii baba alipokufa ameingia Uswisi na kuchukua uraia wa nchi hiyo na kujitwalia uongozi wa taasisi akichukua fedha nyingi za wafadhiri kwa mba anasaidia wanakijiji lakini kiasi anchochukua na feha inayofika kwenye taasisi ni tofauti.’’anasema.

Shari anaongeza kuwa  shangazi yake amejawa na tama amekuwa akilalamikiwa kufanya mambo yasiyo faa kwenye jamii ikiwemo kuukana uraia wa nchi yake akijifanya mfadhiri wa Taasisi ya kaka yake kwa le ngo la kutafuta mlango wa ulaji fedha huku akiomba Rais Dr,Samia aingilie kati ili mama yake aishi kwa amani.

Akizungumza huku akitokwa na machozi,Mjane Mariam Kalupande (63) anasema kitendo anacho fanyi wa na wifi yake Lovina Kalupande  aliyemlea na kumsomesha kupokonya mali akitumia nguvu ya pesa na ameyafanya maisha yake na familia yake kuwa ni ya hofu kubwa .

Kaka yake Mzee Kalupande  ni Mumewe aliyepewa eneo na babu yake na serikali ya kijiji ilimpatia hati miliki alishangaa kuona Mkuu wa wilaya wakati huo John Palingo kuipokonya hati lakini baada ya kwenda mahakamani ameshinda kesi lakini bado anapata vitisho.

Anasema alinyanyasika sana wakati afisa tarafa ya Vwawa  wakati huo Haji Hamis aliyehamishiwa tarafa ya Kamsamba ambaye alikuwa hamtendei haki akidai alikuwa akimkandamiza kwa kila jambo wkati akiitetea ardhi yake na familia,ambaye pia na yeye ni mjumbe wa bodi ya taasisi hiyo,’’Nataka kwenda Ikuru kwa Rais Dr,Samia anisaidie’’.

Anasema mumewe wakati anafariki aliacha matrekta mawili,Gari aina ya Toyota moja na vifaa vingine ambavyo Rovina alivihamisha kinyemela na ilipofika April 28/2023 alishangaa kuona askari 6 mgambo wa kampuni ya ulinzi iliyopo stendi kuu walifika na kuweka kambi zilipo ofisi.

Anasema baada ya kukaa siku kadhaa walinzi hao,alishangaa kuona miche ya kahawa imekatwa ndipo alipoenda polisi na watu hao kukamatwa na kuwekwa lumande na siku ya tatu walitolewa na hadi leo hawachapelekwa mahakamani.

‘’Kama amefanikiwa kuchukua mali za taasisi,aniachie ardhi ya mume wangu kwani ardhi ilianza kumilikiwa ndipo taasisi hiyo ilifuatwa na muasisi ni mume wangu akishirikiana na fafiki yake raia wa Uswisi ambao wote wamekufa na kuzikwa kwenye eneo hilihili ,naomba Rais Samia anisaidia’’anasema.

Kwa upande wake Rozina Kalupande,anasema lile ni eneo la shamba wala si mali ya kaka yake na kuhusu taasisi kaka yake alikuwa ni kiongozi tu wala hakuwa mmiliki licha ya kuwa yeye ndiye aliyeanzisha  kwani mali ni za Taasisi na si za mtu binafsi.

Anasema tuhuma walizompasi za kweli kwani ngekuwa anafanya mambo yasiyofaa serikali ingemchukulia hatua na kwamba yeye kwa sasa anauraia wa Uswisi na anaifadhiri taasisi hiyo.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu ,mkuu wa wilaya ya Mbozi Ester Mahawe,anasema Rovina alifika ofisini kwake kuzungumzia mambo ya ujenzi wa vyoo vya kijiji na kwamba hafahamu zaidi kuhusu mjane huyo hivyo ameahidi akirudi ofisini atalifanyia kazi sakata hilo.

SHERIA YA ARDHI NA MAAMUZI YA MAHAKAMA YALIVYOTOLEWA.

Mahakama ilimpa ushindi marehemu Kalupande katika sesi iliyofunguliwa na Kiongozi wa WAKINA ambapo upande wa mlalamikaji mawakili wa serikali ambao ni Razoaro Mwakimenya na Jerry January ndiyo walisimamia huku upande wa Kalupande ilisimamiawa na ofisi ya mawakili BAISTAR chini ya Amon Nyingi na Mka Mbise.

Mahakama ilimpa ushindi Leston Kalupande ilizingatia kifungu  ch 3 {1} {c} na {g} cha sheria ya ardhi ya vijiji sura ya 114 kama ilivyofanyiwa marejeo  mwaka 2019.

Na pia uneweza kuangalia amri ya 1 ya kanuni ya 10 (2) ya sheria ya muenendo wa madai (cpc) sura ya 33 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2019.



 Wakiwa eneo walilozikwa waasisi wa Taasisi ya wakina .
Kwa mantiki hii inaelezwa kuwa mali ya Leston Kalupande wengine ni wavamizi kwani hati na upimaji uliofanyika ubatilishwe kwani ulifanyika juu ya hati ya mtu mungune.

Ushahidi uliotolewa upande wa Kalupande haukutia shaka,kwani kifungu cha 65 (1) ch sheria ya ushahidi sura ya 6 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2022 mdaiwa namba moja hajadhibitisha kama alipata hati miliki ya kimila kihalali.

Ushahidi uliotolewa kwamba eneo hilo halina hati miliki ni dhaifu ,kwani Kalupande alipewa eneo hilo na babu yake Shangala Halinga mwaka 1985 na kuanza kujenga majengo ndipo taasisi hiyo ilianzishwa kwenye majengo hayo.

Kutokana na uwepo wa migogoro ya aina hii inayotishia na kuhatarisha maisha ya watu,ipo haja Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzani Dr,Samia Suruhu chini ya wizara ya ardhi kuingilia kati kuhepuka machafuko hasa kwenye eneo hili la mjane wilayani Mbozi.




Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa