Wafanyabiashara wa minadani waonywa kupanda malori bali wapande mabasi ya abiria
Na Israel Mwaisaka,Nkasi
KAMANDA wa Polisi mkoani Rukwa Shadrack Masija amewataka Wafanyabiashara za minadani kuacha mara Moja kupanda magari ya mizigo wanapokwenda kwenye biashara zao Bali wajitenganishe na mizigo kwa kupanda mabasi ya abiria.
Akizungumza na Wananchi wa wilaya Nkasi Leo chini ya Programme ya Polisi jamii kupitia mazoezi ya utimamu (Jogging) amesema kuwa kumekuwepo na utamaduni wa Wafanyabiashara wa kupanda magari ya mizigo kwenda minadani na kuwa wengi wamefariki au kujeruhiwa inapotokea ajali na kuwa sasa iwe mwisho kufanya hivyo na kinachotakiwa sasa ni kuisafirisha mizigo kwenye maloli na wao wasafiri kwenye mabasi ya abiria kufuata mizigo Yao.
Alisema kuwa ni kosa kubwa kwa Wafanyabiashara kuchanganyana na mizigo kwenye maloli na kuwa maelekezo yalikwishatolewa kwa viongozi wao na kuwa atakayeendelea kupanda kwenye mabasi atakua anakaidi maagizo halali ya serikali na kuwa hayo yanalenga kuwafanya Wafanyabiashara wanakua salama wakati wote kutokana na umuhimu wao katika jamii.
Sambamba na Hilo ameagiza Wafanyabiashara za mifugo kuhakikisha kuwa Kila mnyama anakuwa na kibali chake na kuachana na ule utamaduni wa kuuza ng'ombe 20 kwa kibali kimoja na kuwa sasa ukikamatwa una kibali kimoja wakati una mifugo mingi utakamatwa na kufikishwa mahakamani kwa kosa la wizi wa mifugo.
"Ni mwiko kuuza mifugo mingi kwa kibali kimoja ukiwa na Mbuzi 20 Kila Moja iwe na kibali chake,Ng'ombe 10 Kila Moja awe na kibali chake na hats kwa mfanyabiashara wa bucha tukimkuta anauza nyama ya Ng'ombe tuone kibali Cha Ng'ombe huyo na SI kusema nilinunua kwa kibali kimoja kwa Hilo hatutaelewana" alisema Kamanda Masija.
Mwenyekiti wa Wafanyabiashara za minadani Samsoni Njeyanje kwa upande wake amesema kuwa agizo Hilo wao kama Wafanyabiashara walishaanza kulitekeleza na kuwa malori yamewaumiza sana Wafanyabiashara kwa maana wengi wamepoteza maisha na wengine wengi kupata ulemavu wa kudumu na kuwa Toka waanze kuitekeleza Sheria hiyo ajali zimepotea kabisa na wao sasa wapo salama .
Alisema kuwa wengi ya Wafanyabiashara walikua wanapanda malori kuchanganyana na mizigo wakidhani kufanya hivyo ni kubana bajeti lakini matokeo ya ajali,vifo na ulemavu uliokuwa unawapata pale inapotokea ajali kumewafanya wenyewe kuona umuhimu wa kupanda kwenye mabasi ya abiria na kujiona wapo salama kwa sasa.
Pia mkaguzi msaidizi wa Polisi wilayani Nkasi Masud Bakari alidai kuwa dhana ya Polisi jamii imelenga kusogeza huduma ya ulinzi kwa jamii Ili kuweza kuwafichua wahalifu kwa haraka na kufikishwa kwenye vyombo vya Sheria na kubwa ni kutaka kuona uhalifu unadhibitiwa hats kabla ya kufanyika.
Na aligusia na suala la ukatili wa kijinsia ambapo alidai kuwa hivi karibuni zimemalizika siku 16 za kupinga ukatili na kuwa ukatili unafanyika ndani ya jamii na kuomba kwa Kila Moja kuwajibika kwa kutoa taarifa kwenye mamlaka husika Ili kuweza kukabiliana na vitendo hivyo vya ukatili.



Comments
Post a Comment