Na Israel Mwaisaka,
Sumbawanga

SERIKALI wilayani Nkasi Mkoani Rukwa imewaonya watendaji wa idara ya elimu kutoweka vikwazo vitakavyo sababisha baadhi ya watoto waliofikia umri wa kuanza elimu ya awali na darasa la kwanza wakakosa fursa hiyo.

Mkuu wa wilaya hiyo, Peter Lijualikali alitoa agizo hilo jana wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya mkuu wa mkoa, juu ya mafanikio ya utekelezaji wa miradi katika sekta ya Elimu, Afya na Maji ambapo alisema kuwa miradi yote imekamilika kwa zaidi ya asilimia 95.

Alisema kuwa hivi sasa ni wakati wa kuandikisha watakao anza elimu ya awali na shule ya msingi hivyo hataki kusikia mtoto yoyote ameshindwa kuanza shule kwasababu ya michango ama cheti cha kuzaliwa kwani kunataarifa zisizo rasmi kuwa mtoto atakae kosa cheti hicho hata andikishwa shule.

"Natoa Onyo kwa walimu wakuu na watendaji wengine wa elimu kutodai michango yoyote kwa mzazi anaye mwandikisha shule mtoto wake kwani serikali imeshajenga madarasa imeweka madawati na vifaa vyote vya elimu hivyo sitaki kusikia michango inakua kikwazo, wala cheti cha kuzaliwa kisiwe sababu ya mtoto kukosa fursa ya elimu" alisema Lijualikali.

Kuhusu miradi iliyotekelezwa wilayani humo mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa katika mwaka wa fedha 2022/2023 wilaya hiyo ilipokea tsh Bilioni kumi ambazo zimejenga na kukarabati shule, zahanati, vituo vya Afya pamoja na miradi ya maji ambayo imeondoa kero kwa wananchi.

Aidha alisema kuwa fedha za miradi zilizotolewa na serikali kuu katika mwaka wa fedha 2023/2024 tayari zimepokelewa wilayani humo na baadhi ya miradi ya maendeleo imeanza kutekelezwa na ipo katika hatua mbalimbali hasa maeneo ya pembezoni ya wilaya hiyo ambayo itatatua kero kwa wananchi wa maeneo hayo.

Hata hivyo Lijualikali alimshukuru Rais Wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Hassan kwa uongozi wake madhubuti unaowezesha kupatikana fedha zinazo tekeleza miradi ya maendeleo ambayo itatatua changamoto zinazo wakabiri wananchi wa wilaya hiyo.



Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa