Wananchi kata ya Mkinga wajenga ofisi tano za kisasa za vijiji kwa kujitolea
Na Israel Mwaisaka, Nkasi
Kamati ya maendeleo ya kata (WDC) kata ya Mkinga wilayani Nkasi mkoani Rukwa imefanikiwa kuwahimiza Wananchi kujenga ofisi za Kijiji za kisasa kwa Kila Kijiji kwa njia ya kujitolea na ofisi hizo kukamilika.
Akizungumza na Waandishi wa habari Diwani wa kata hiyo Mohammed Zaid alisema kuwa mpango huo uliazimiwa kwenye vikao vya maendeleo ya kata na Wananchi wakaupokea mpango huo kwa moyo mmoja na kuanza utekezaji wa mpango huo
Alisema kuwa viongozi wa vijiji waliamua kuusimamia mpango huo kwa weredi ambapo waliweka utaratibu wa uchangishaji wa Fedha ikiwa ni pamoja na nguvu za Wananchi.
Alisema kuwa kutokana na jitihada zilizoonyeshwa na Wananchi halmashauri kupitia mfuko wa jimbo iliamua kusapoti jitihada hizo kwa Kutoa mifuko 20 ya saruji kwa Kila kijiji ambazo zilitumika kwenye umaliziaji wa ujenzi na kufanikiwa kuwa na ofisi nzuri na za kisasa kwa Kila Kijiji.
Awali Mwenyekiti wa Kijiji Cha Mkinga Alex Maziku alidai kuwa ofisi zao za Kijiji zilikua na hari mbaya kiasi Cha wao kusukumwa kupitia vikao vya maendeleo ya kata na kulazimika kutoka na maazimio ambayo Sasa mafanikio wameyaona kwa kuwa na ofisi ya kijiji.
Alisema kuwa Wazo hilo lilianza kwa ugumu na kuona kana kwamba hawawezi kufanikiwa lakini walishangazwa na moyo wa Wananchi waliouonyesha na wao kama viongozi walitengeneza mazingira ya uwazi ambapo Wananchi walikua wanaona matumizi sahihi ya Fedha zao walizokuwa wakichanga na kuridhishwa nao.
Afisa mtendaji wa Kijiji Cha Mkinga Edisi Mbalamwezi amedai kuwa ofisi yake ya Kijiji ilikua na mazingira magumu na kuwa Sasa anafanya kazi katika mazingira bora hasa la Wananchi kuhudumiwa katika mazingira mazuri na salama.
Alisema moyo waliouonyesha Wananchi wa kujitolea kwa moyo uliwafanya na wao kama viongozi kuongeza bidii ikiwa ni pamoja na uwazi na kuwa hilo limekua ni moja ya mafanikio waliyoyapata Katika kufanikisha mpango huo muhimu kwa maendeleo ya kata Yao ya Mtenga.
Kata ya Mkinga imejidhatiti kwa kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya ujenzi wa kituo Cha afya Mkinga,ujenzi wa Stand ya mabasi na Kituo Cha afya katika mwaka huu wa Fedha wa 2026/27.
Diwani wa kata hiyo Mohammed Zaid amedai kuwa licha ya Wananchi kuamua kujitolea kwa moyo katika ujenzi wa miradi hiyo bado wanahitaji msaada mkubwa kutoka serikalini na kubwa kwa Sasa ni la ujenzi wa Kituo Cha afya na kuwa kulingana na mazingira ya kata hiyo Kuna ulazima mkubwa wa Kituo Cha afya katika kata hiyo.





Comments
Post a Comment