DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI
Na Israel Mwaisaka,Nkasi
DIWANI wa kata ya kala Wilayani Nkasi Privatus Yoramu (CCM) amefariki Dunia baada ya kuugua kwa muda mfupi .
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya Nkasi Richard Maasai ni kuwa tukio hilo limetokea Juzi jumatano majira ya saa 12 jioni wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya mkoa Rukwa.
Amesema kuwa marehemu amefariki kutokana na ugonjwa wa kiharusi na ugonjwa huo aliupata kutokana na ugonjwa uliokuwa umempata wa shinikizo la juu la damu (Pressure) na kupelekea mishipa ya damu kupasuka na hatimaye kupata ugonjwa wa Kiharusi uliopelelea umauti wake.
Mwenyekiti huyo wa halmashauri amefafanua kuwa majuzi aliongoza kikao Cha kamati ya elimu na afya kama Mwenyekiti na akiwa katika kikao hicho alizidiwa na ugonjwa na kukimbizwa katika hospitali ya Wilaya Nkasi ambapo alipewa huduma ya awali na kukimbizwa katika hospitali ya mkoa kwa matibabu zaidi .
Na amedai kuwa mazishi ya Diwani huyo yatafanyika kesho jumamosi ya wiki hii ya tarehe 31 katika Kijiji Cha Kilambo Cha Mkolechi kata ya Kala.

Comments
Post a Comment