"MTENGA WE ARE TOGETHER" KUNDI LA WALIOSOMA SHULE YA MSINGI MTENGA WACHANGIA MADAWATI 20





Na Israel Mwaisaka, Nkasi
‎Umoja wa Watu waliosoma katika shule ya msingi Mtenga wajulikanao " Mtenga we are together"wamechangishana na kutengeneza madawati 20 yenye thamani ya zaidi ya Mil.1.8 na kuyakabidhi shuleni hapo kama sehemu ya kupunguza tatizo la uhaba wa madawati katika shule hiyo.
‎Akizungumza wakati wa kukabidhi madawati hayo jana Jumanne Januari 20,2026 mwakilishi wa umoja huo Alexander Romwad Kapele amesema kuwa wao kama Watu waliowai kusoma katika shule hiyo wametengeneza umoja wa kusaidiana katika shida na raha na wakaona ipo haja kwao kusaidia shule hiyo walau kwa madawati wenye uwezi nayo.

‎Amesema kuwa umoja huo wenye wanachama 40 waishio katika mikoa mbalimbali hapa Nchini walihafiki wazo hilo na kuamua kutengeneza madawati hayo 20 ili kuweza kupunguza tatizo la uhaba wa madawati katika shule hiyo ili Watoto waweze kusoma katika mazingira mazuri na salama.
‎Akipokea madawati hayo mwalimu Mkuu wa shule hiyo Osiana Mgala ameushukuru umoja huo wa Watu waliosoma katika shule hiyo kwa kuikumbuka shule hiyo na kuweza kutoa msaada huo ambao anaamini utawasaidia Watoto wengi waliokuwa wakikaa chini .


Amedai kuwa shule hiyo yenye Wanafunzi 1,327 kwa Sasa Ina uhaba wa madawati 251 ambapo mahitaji ni 456 na yaliyopo ni 205 na kuwa bado wanauhitaji mkubwa wa madawati na kuwaomba Watu wengine wenye uwezo wa kusaidia waendelee kujitokeza kama walivyofanya kundi hilo la "Mtenga we are together"
‎Mwalimu Mkuu huyo amedai kuwa madawati hayo yatapelekwa katika darasa la pili na madarasa mawili la kwanza na la pili ndiyo yenye uhaba mkubwa wa madawati na kuwa amependekeza darasa hilo la pili kupewa madawati hayo kwa sababu mwaka huu Wanafunzi wa darasa hilo ni watahiniwa.


‎Mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo Patrick Dominico ameushukuru umoja wa Mtenga we are together kwa wazo hilo la kusaidia shule hiyo madawati na kuwa wamesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza tatizo hilo la madawati na kuwaomba wadau hao wasichoke kusaidia kama hivyo pale watakapokuwa wanapata uwezo.
‎Amedai kuwa shule hiyo bado Ina changamoto kubwa ya madawati na uchakavu wa baadhi ya majengo na kuwa inahitajika nguvu kubwa katika kurekebisha miundo mbinu hiyo,hivyo misaada
‎Afisa elimu wa kata hiyo ya Mtenga Benedicto Msesa amedai kuwa jambo hilo lililofanywa na Mtenga we are together ni la kuigwa kwa Watu wote na kama mawazo hayo yataambukizwa kwa makundi mengine ya kijamii italeta faraja kubwa kwa jamii nzima ya kata ya Mtenga.

‎Diwani wa kata hiyo Frank Helandogo na afisa mtendaji wa kata hiyo Adela Selemani wamedai kuwa wao wanayakaribisha makundi mengine ya kijamii kwa misaada kama hiyo na zaidi ya hapo kwa maendeleo ya jamii nzima ya Mtenga,Wilaya, mkoa na hata taifa kwa ujumla.

Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa