WATUMISHI NKASI WAPIGWA MSASA JUU YA UANDAAJI WA MIPANGO NA BAJETI.





Na Asha Hassan,Nkasi

Katika jitihada za kuimarisha ufanisi wa matumizi ya rasilimali za umma na kuhakikisha kuwa vipaumbele vya maendeleo vinatekelezwa ipasavyo, Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa, leo October 13, 2025 imeendesha mafunzo maalum kwa watumishi wake kuhusu uandaaji wa mipango na bajeti.

Mafunzo hayo yalilenga Kuwajengea uwezo watumishi, wakuu wa idara na vitengo wa halmashauri kuelewa mchakato wa kupanga bajeti kwa njia sahihi, mafunzo yaliyoendeshwa kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo.


Aidha katika mafunzo hayo wawezeshaji lakini pia ni Maafisa Mipango Wilaya ya Nkasi, Ajaye Nguvila na Renatus Panda walisema dhumuni kubwa la mafunzo hayo ni Kufundisha mbinu za kuandaa mipango ya shughuli (action plans) zinazoweza kutekelezeka ndani ya bajeti

Sambamba na hayo Kutoa ufahamu juu ya mfumo wa kitaifa wa mipango na bajeti (kwa mfano system za PlanRep).


Mafunzo hayo yalifanyika kwa ushirikiano kati ya idara ya mipango ya Halmashauri yakihusisha Wakuu wa idara na vitengo, ambapo Mafunzo yalijumuisha mafunzo ya nadharia na vitendo .


Kwa upande wa Watumishi walioshiriki mafunzo hayo wamesema wamepata uelewa juu ya  mchakato na uandaaji wa bajeti na mipango, hivyo kuongeza uwezo wao wa kuandaa bajeti bora kupitia Idara na vitengo vyao.


Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa