WAKAZI 9594 WA VIJIJI 3 KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI MWENGE WA UHURU UKIRIDHISHWA.



Na Ibrahim Yassin, Momba

WAKAZI 9594 wa vikiji vya Tontela, Kaonga na Nzazya kata ya Chirurumo wilayqn8 Momba mkoani Songwe wametoa tabasamu lao mbele ya kiongozi wa mbio za mwenge wakifurahia maji safi.

Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira (Ruwasa) wilayani Momba inatekeleza ujenzi wa mradi wa maji Tontela _Kaonga na Nsazya kwa kutumia fedha za lipa kwa matokeo (P4R).



Kazi za mkataba huu zinatekelezwa na mkandarasi M/S KGG Investment kwa thamani ya Tshs ,1,985,103,643.14 .

Mradi huu unatarajia kutoa huduma ya maji kwa wakazi 9594 katika vijiji vya Tontera, Kaonga na Nsanzya kata ya Chilulumo.

Mpaka sasa mkandarasi ametekeleza ujenzi wa tenki la maji lenye ujazo wa lita 150,000 na mnara wa mita 9 ,ujenzi wa nyumba ya mitambo,,ofisi ya chombo cha watoa huduma za maji ngazi ya jamii na uchimbaji wa mtaro. 

Pia kazi nyingine ni ulazaji mabomba kilometa 27 ambapo kiasi cha fedha kilicholipwa ni Tsh, 327,204,688.94 na kiasi ambacho bado hakijalipwa ni Tsh, 923,266,546.47.


Hata hivyo kukamilika kwa mradi huu kutaondoa changamoto ya maji ambayo inawakabili wananchi kwa kupunguza umbali mrefu wa kwenda kuchota maji mto Momba na kuondokana na hatari ya kukumbwa na magonjwa ya milipuko.

Meneja wa Ruwasa wilaya ya Momba Mhandisi Beatus Katabazi amesema anaipongeza serikali kwa kutoa fedha hizo kwani  imesaidia kutatua changamoto hiyo .

Amesema mradi huo una vituo 15 vya kuchotea maji likiwa na tenki lenye ujazo wa lita 150 na mtanda o wa Bomba eneo la mradi ni kilometa  27.

Baada ya kukagua mradi huo kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Ismail Ally Ussi, ameupongeza mradi huo na kusema kuwa fedha za serikali zimetumika vizuri.


Hata hivyo wakazi wa eneo hilo wakiongizwa na Safia Mwashilindi amesema kukamilika kwa mradi huu kumewapunguzia hadha ya kutembea umbali mrefu kusaka maji katika mto momba ambayo hata hivyo si safi na salama.

Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa