TUNDUMA YAELEZA MAFANIKIO MAPAMBANO DHIDI YA MALARIA .
Na Ibrahim Yassin, Tunduma.
Halmashauri ya mji Tunduma, yaeleza mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria kwa mkimbiza mwenge wa uhuru kitaifa pamoja na mikakati yake.
Grece Malunu akizung umza kwaniaba ya mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Mariam Chaurembo ni kuwa maambukizi ya ugonjwa huo yapo chini ya asilimia 4.
Amesema wamefikia hatua hiyo kutokana na hafua zilizotolewa na zinaendelea kutek elezwa hadi sasa .
Afua hizo ni kununua jumla ya viua dudu lita 500 zenye tham ani ya Tsh, 6,000,00 0.00 zilizotumika na zinaendelea kutumika.
Amesema pia ulifanyika ugawqji wa vyandarua 9,093 vyenye thamani ya Tsh, 90,930,000.00 vilivyogawiwa katika vituo 25 vya afya .
Amesema sababu nyingine iliyowqpa mafanikio ni utoaji elimu na matumizi sahihi ya vyandarua ambapo bado wanaen delea kugawa.
Amesema mwaka 2023/24 kulikuwa na vifo 6 ambavyo vimepunguq hadi vifo 4 mwaka 2024/2025 .
Amesema pia kuongez eka kwa maeneo yali yofikiwa na huduma ya upuliziqji wa dawa za viuadudu vya Mala ria kutoka madimbwi 16 mwaka 2023 hadi madimbwi 42 mwaka 2025.
Amesema kwa kipindi cha januari hadi Juni 2025 wateja 50,996 walihudumiwa 20.422 walipimwa vimelea kati ya hao 1,330 walikutwa na vimelea sawa na asilimia 6.5 .
Amesema pia wajaw azito 18 kati ya Waj awazito 6,135 waliop imwa waliogun dulika kuwa na vimelea vya Malaria na kutibiwa.
Amesema watoto 3,930 waliopatiwa chanzo ya surua na waliopokea vyandarua ni 3,270 sawa na asilimia 85 na kuwa jitihada zinaen delea kufanyika.
Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Ismail Ally Ussi amesema ameupongeza uongozi wa halmashauri hiyo kwa kazi nzuri ya mapambano dhidi ya Malaria.





Comments
Post a Comment