POLISI RUKWA WAJIPANGA KUIMARISHA USALAMA SIKU YA UCHAGUZI MKUU






Na Israel Mwaisaka,Rukwa

Kamanda wa Polisi mkoani Rukwa SACP  Shadrack Masija  amewatoa hofu Wananchi juu ya usalama wao kipindi cha kupiga kura na baada ya uchaguzi kwani jeshi hilo limejipanga vizuri katika kuhakikisha suala la usalama linakuwepo wakati wote.

Akizungumza na Wananchi kupitia Radio moja ya kijamii Nkasi FM jana kamanda Masija amesema kuwa Wananchi wasiwe na hofu katika kipindi chote cha uchaguzi juu ya usalama wao na kuwataka wajitokeze kwenda kupiga kura ikifika tarehe ya kupiga kura bila ya hofu yoyote juu ya usalama wao.

Alisema kuwa katika kipindi hiki cha kueleke uchahuzi mkuu mkuu ni wakati wa kila mmoja kufuata kanuni kam tunavyoelekezwa na sheri za Nchi ikiwa ni pamoja na maelekezo ya tume huru ya taifa ya uchaguzi ili kuweza kushiriki uchaguzi bila ya kuvunja sheria za Nchi.

Alidai kuwa jeshi la Polisi ndiyo lenye dhamana la kuhakikisha usalama wa raia na mali zake unakuwepo wakati wote hivyo ni jukumu lao kuhakikisha usalama unakuwepo na kuwaomba Wananchi kutoa ushirikiano kwa Polisi pale wanapoona kuna dalili ya uvunjifu wa amani popote pale watakapokuwepo.

Pia Kamanda Masija amewataka Wananchi siku ya uchaguzi wasiogope baada ya kuwaona Polisi wengi kwenye vituo vya kupigia kura na hata  barabarani kwani wapo kwa ajili ya kulinda usalama wao na mali zao na wanatakiwa watembee vifua mbele.

Na amewataka Watu watakaopiga kura siku hiyo wakishapiga kura waondoke kwenye vituo vya kupigia kura waende nyumbani kuendelea na majukumu mengine huku wakisubiri matokeo na kazi ya kulinda kura ni jukumu la Mawakala wa vyam ikiwa ni pamoja na Polisi.

Sambamba na hilo kamanda Masija amedai kuwa katika majukumu yao ya ulinzi wa amani wamefanikiwa kuwakamata vijana 20 na kuwafikisha mahakamani kwa makosa ya utapeli kwa njia ya mtandao ya Tuma kwenye namba hii.

Amesema kuwa lengo lao sasa ni kukabiliana na vitendo hovyo vya utapel ambapo kw mujibu wa TCRA mkoa Rukwa umeshika nafasi ya pili kwa utapeli kitaifa ikiongozwa na mko w Morogoro.

Amefafanua kuwa vitendo vya utapeli vinawaacha watu katika umaskini baada ya kutapeliwa na kuwa jambo hilo wamelivalia njuga ili kuweza kukomesha vitendo hivyo vya kitapeli.


Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa