MZEE AJINYONGA KWA KAMBA YA KATANI AACHA MASWALI
Na Israel Mwaisaka,Nkasi
MZEE Jelas Lunguya (75) mkazi wa Kijiji Cha Nchenje kata ya Kate wilayani Nkasi amefariki dunia baada ya kujinyonga.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na afisa mtendaji wa Kijiji Cha Nchenje Salome Auseni Ni kuwa tukio Hilo limetokea usiku wa kuamkia leo Ijumaa ambapo mzee huyo alikutwa amefariki kwa kujining'iniza kwenye mti kwa kutumia kamba ya katani.
Amedai kuwa mti huo alioutumia kujinyonga upo nje kidogo ya nyumba yake na unajulikana kwa jina la Mchese na hadi Sasa haiujulikani chanzo Cha tukio hilo.
Mtendaji huyo amefafanua kuwa tukio Hilo la mzee huyo kujinyonga limeacha maswali mengi kwa jamii na familia yake kwa maana kwamba hawajawai kusikia mgogoro wowote wa kifamilia ambao unaweza kupelekwa mtu kuchukua maamuzi magumu Kama hayo.
Amesema kuwa marehemu amezikwa baadae ya taratibu za Kipolisi kukamilika.
Mkuu wa wilaya Nkasi Peter Lijualikali amethibitisha kutokea kwa tukio Hilo na kudai kuwa uchunguzi zaidi unaendelea juu ya tukio hilo

Comments
Post a Comment