MWENGE WA UHURU WAZINDUA BARABARA ILIYOAHIDIWA NA HAYATI MAGUFULI ,TARURA YAPONGEZWA



Na Ibrahim Yassin ,Songwe.

Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Ismail Ally Ussi amepongeza wakala wa barabara mijini na vijijini (Tarura) mkoani hapa jinsi walivyojenga kiufanisi  barabara ya Mkwajuni makao makuu ya wilaya. 

Barabara hiyo ya mkwajuni kilometa 4.0  iliahidiwa na akiyekuwa Rais wa awamu ya tano hayati John pombe magufuli na imetekelezwa na Rais wa awamu ya sita Dkt, Samia Suluhu. 

Ujenzi huo ulianza kilometa 2.0 mnamo tarehe 4/8/2024 na kukamilika Oktoba 25/2025 kwa thamani ya Shilingi Milioni 760. ambapo hadi sasa shilingi Milioni 591,262,775 zimetumika sawa na asilimia 78.


Kwa mujibu wa meneja wa wakala wa barabara mijini na vijijini (Tarura) wilayani Songwe mhandisi Emmanuel Nkwera ni kwamba ujenI huo umetekelezwa kwa awamu mbili.

Amesema awamu ya kwanza walianza kujenga mifereji sehemu korofi na awamu ya pili ilikuwa ni kujenga makaravati na kuchora mistari sambamba na uwekeji wa taa. 

Amesema fedha za ujenzi wa.mradi huo zimetokana na tozo za mafuta ambapo mradi huo upo Tarafa ya Kwimba kata ya Mkwajuni wilayani Songwe. 



^Ndugu kiongozi wa mbio za mwenge hadi sasa barabara zilizojengwa kwa kiwango cha Lami ni kilometa 4.87.

Amesema. Barabara hiyo imeongeza fursa za kiuchumi kwani wakasilia mali sasa wanafanya biash ara hadi usiku na hata mji wa mkwajuni umekuwa kama Dar es Salaam ndogo.

"Tulianza kujenga kilometa Mbili na sasa tunajenga kilometa mbili na kuufanya mji huo kuwa na barabara za Lami kilometa 4.87 " amesema mhandisi Nkwera. 



Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Ismail Ally Ussi amesema barabara hiyo imepokelewa huku akiwasifu viongozi wa Tarura kwa umakini katika utekelezaji wa mradi huo.



Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa