MWENGE WA UHURU WARIDHISHWA NA MRADI UJENZI WA MADARASA MOMBA.
Na Ibrahim Yassin, Momba
MWENGE wa uhuru umeridhishwa na ujenzi wa vyumba 4 vya madarasa na ofisi mbili shule ua msingi Malangwa.
Shule hiyo ya msingi ipo katika kijiji cha Kamsamba ilianzishwa mnamo tarehe 15/2/2019 ikisajiliwa kwa namba EM.18218 ikiwa na wanafunzi 60.
Shule hiyo ilikuwa na changamoto nyingi lakini serikali ya awamu ya sita kwa kushirikiana na wananchi wa eneo hilo walijenga madarasa hayo kutatua changamoto iliyopo.
Kwa mujibu wa taarifa ya Nyerere Nzunda aliyoisoma kwaniaaba ya mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo amesema wamefanikiwa kukamilisha ujenzi wa.madarasa manne na ofisi mbili .
Amesema mradi huo uligharinu Tsh,Milioni 104,550.000.00 ambapo Tsh 100,000,000.00 zilitola serikali kuu na Tsh, 4,550,000.00 ni thamani ya nguvu za wananchi kwa kuchimba mtaro, kusafisha eneo na kuchota maji.
Amesema mrqdi huo ulianza kutekelezwa Juni 7/2025 na umekqmilika Septemba 9/20/2025 ukijengwa kwa force account umepunguza uhaba wa madarasa.
Hata hivyo amesema anaipongeza serikali kwa kutoa kiasi hicho cha fedha kilicho saidia kuondoa changamoto hiyo ya wanafunzi.
Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Ismail Ally amesema ameridhishwa na mradi huo baada ukaguzi wa nyaraka kisha akaendelea na ukaguzi wa miradi mengine.

Comments
Post a Comment