MWENGE WA UHURU KUKAGUA MIRADI YA BIL 20.5 .WANANCHI WAKIASWA KUJITOKEZA KUPIGA KURA.

                                      MAKALA
-RAIS DKT,SAMIA KUUZIMA MWENGE WA UHURU MKOANI MBEYA SIKU YA NYERERE DAY.


Na Ibrahim Yassin. Songw

Mwenge wa uhuru  umekagua miradi 43 yenyethamani ya Tsh,Bilioni 20.5 katika wilaya 4 Halmashauri 5 Mkoani Songwe ambapo umetembea kilometa 634 na utazimwa siku ya sikukuu ya Nyerer Day mkoani Mbeya..

Mwenge huo wa uhuru ulipokelewa siku ya Oktoba 2/2025 katika kijiji cha Chitete kata ya Chitete bonde la Kamsamba wilayani Momba mkoani Songwe ukitokea mkoani Rukwa. 


Akikabidhi mwenge huo kwa mkuu wa mkoa wa Songwe, mkuu wa mkoa wa Rukwa Charles Makongoro  Nyerere anasema mwenge huo ulikagua na kuzindua miradi ambayo yote imekubaliwa pasipo kuwa na kasoro..


Nyerere ansema katika wilaya zote nne za mkoa wa Rukwa mwenge huo ulikagua miradi  yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 55 ambayo ilikaguliwa na mingine iliwekewa mawe ya msingi. 



Anasema mwenge huo ulio asisiwa na wazee baba wa Taifa Hayati mwalimu Julias Nyerere na Hayati Abeid Aman Karume lengo kuu ni kumulika penye kiza kuleta upendo na utulivu penye chuki,na ni alama ya ukombozi wa nchi.


Akiupokea mwenge huo, mkuu wa mkoa wa Songwe  Jabir Omary Makame amesema mwaka 2024 mwenge huo ulikagua miradi 46 yenye thamani ya Bilioni 18 lakini mwaka huu 2025 mwenge huo utakagua miradi 43 yenye thamani ya Bilioni 20.5.


anasema miungoni mwa miradi hiyo ni ya afya,elimu,maji,miundombinu na miradi mingine huku akimueleza mkimbiza mwenge kuwa katika ujaguzi huo wapo tayari kupokea maelekezo.


Anasema serikari ya awamu ya sita ilifanya kazi kubwa ambapo fedha zaidi ya Bilioni 7013 zilitolewa kujenga miradi ya maendele na kuufanya mkoa huo kung'ara .




Anaongeza kuwa mkoa wa Songwe ni lango la nchi za kusini mwa Afrika (Sadc)  hivyo wao kama viongozi wameisimamia ipasavyo Ilani ya Chama cha Mapinduzi  chini ya mwenyekiti Dkt,Samia Suluhu.


Anasema kubwa kabisa ni ukaguzi wa daraja muhimu la msangano katika mto Nkana ambalo limetumia Bilioni 3 na lipo asilimia 80 ya ujenzi.


Anasema daraja hilo likikamilika litakuwa mkombozi wa wakazi wa bonde la msangano na kurahisisha safari ya kutoka bonde hilo la msangano na kamsamba kwenda Tunduma.


Anasema daraja hilo wakati wa mvua za masika wananchi walilazimika kuvuka kwa kutumia mtumbwi wakilipa 7.000 kwenda upande wa pili hali iliyoumiza uchumi wa wananchi.


anasema kwa usumbufu huo serikali ya awamu ya sita iliwafuta machozi wananchi kwa kutoa fedha Bilioni 3 kujenga mradi huo kuwaondolea wananchi changamoto ya usafiri. 


Anasema mkoa wa songwe ulikuwa ukikabiliwa na uhaba wa maji lakini kipindi cha awamu ya sita karibu kila kata imejengewa mradi wa maji safi na salama.


Anaongeza kuwa kwa upande wa barabara wilaya zote zinapitika pam oja na kwamba baadhi ya wilaya barabara zake ni za vumbi lakini zinapitika baada ya Tarura na Tanroa ds kujenga barabara zote.


Anasema anajisikia faraja kuona kiongozi wa mbio za mwenge kuridh ishwa na miradi iliyokaguliwa amba yo mingine iliwekewa mawe ya msingi.


Anasema tuzingatia ujumbe wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka huu wa 2025 usemao “Uchaguzi mku u wa Mwaka 2025” chini ya kaulimbiu isemayo “Jitokeze kushiriki uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, kwa Amani na Utulivu”. 


“Napenda kutumia fursa hii adhimu kukuhakikishia kwamba sisi Viongozi na Wananchi wa Mkoa wa Songwe kwa umoja wetu tumejipanga kwa dhamira ya dhati kutekeleza kwa vitendo na uadilifu mkubwa ujumbe huu"anasema. 



anasema  kuwa wananchi wote amb ao wanasifa za kushiriki kuchag ua na kuchaguliwa kwa kuzingatia sheri a zilizopo na kanuni zilizotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kwa mwaka 2025 wanashiriki kikamilifu.


Anasema  vyama vyote vyenye usajili wa kudumu na vitakavyo jitokeza kushiriki katika uchaguzi Mkuu vinashiriki bila bughudha zozote na kwa kuzingatia sheria zilizopo.


Kuhamasisha wananchi kujiandikisha katika zoezi la kuboresha taarifa za wapigakura katika daftari la kudumu la wapigakura.


Wananchi wote waliojitokeza katika vituo vya uboreshaji daftari waliweza kuboreshewa taarifa zao kwa hali ya amani na utulivu mkubwa. 


Kuhakikikisha kwamba wagombea walioteuliwa na Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi wanafanya kampeni zao katika mazingira ya amani na utulivu na kwa kuzingatia ratiba za kampeni ambazo zimeandaliwa na Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi.


Anasema watahakikisha wanashiriki ana na Tume huru ya Taifa ya uch aguzi  kuhakikisha kuwa watendaji ambao wameteuliwa kusimamia zoezi la Uchaguzi katika Majimbo 6 ya ubunge na Kata 94 za udiwani wanatekeleza majukumu yao kwa  amani na utulivu.


WAPIGA KURA WAPYA 187323 WAONGEZEKA MKOANI SONGWE.


Akitoa taarifa ya maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 katika mapokezi ya Mwenge wa uhuru,  Jabir Makame mkuu wa mkoa wa Songwe anasema mkoa kwa kushirikiana na tume ya uchag uzi  imeandikisha wapigakura wapya 1,87323 kati ya 1010803 ya awali sawa na asilimia 169 ya uandikishaji.


Rc Makame anaongeza kuwa  wapig akura 70405 waliboresha taarifa zao huku 427 wakifutwa kutokana na ku kosa sifa na kuufanya mkoa huu kw a sasa kuwa na wapigakura 7,62245 waliojitokeza katika vituo vya kujiandi kisha.


Akizungumza mara baada ya kuikag ua miradi hiyo  kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Ismail Ally Ussi anas ema wameikagua na kuweka mawe ya msingi miradi 43  ambayo haina kasoro yeyote.


" ninamfahamu mkuu  wa mkoa makame ,leo ni mara yake ya pili kupokea mwenge huu,mara ya kwanza alipokea akiwa mkuu wa wilaya ya Gairo  na sasa anaupokea akiwa  mkuu wa mkowa wa Songwe, naamini tutapata ushirikiano mzuri "amesema Ussi. 


Anaongeza kuwa Halmashauri zote alizopita ameridhishwa na jinsi zilivyo tumia fedha za mapato ya ndani kuje nga miradi wakitii agizo la serikali na kuagiza mfumo huo.




Ussi mbali na kukagua na kuweka mawe ya msingi miradi 43 mkoani Songwe pia aliwahamasisha wananchi kutumia haki yao ya kikatiba kupiga kura siku Octoba 29/2025.


Mbio hizo za wenge wa uhuru utaitim ishwa mkoani Mbeya Octoba 14 mw aka huu siku ya Nyerere Day na mge ni rasmi atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Samia Suluhu . 






Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa