MWANAFUNZI ALIYEKUFA KWA KUDONOLEWA NA KUKU AZIKWA,BABA MZAZI ASHINDWA KUJIZUIA.
Na Ibrahim Yassin, Mbozi.
MAMIA ya wakazi wa mitaa mbalimbali ndani na nje ya wilaya ya Mbozi mkoani Songwe wajitokeza kuuzika mwili wa mtoto Josiah Benjamin Makelo (12) aliyefariki dunia jana kwa kudonolewa na kuku usiku wa manane.
Katika maziko hayo yaliyofanyika leo Oktoba 13/2025 katika makaburi ya kijamii yaliyopo kata ya Hasanga wilayani Mbozi,wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali,Dini wazee maarufu na raia wa kawaida walishiriki maziko hayo.
Imeelezwa kuwa chanzo cha kifo hicho ni mtoto huyo kudonolewa na kuku mara baada ya kutoka kwenye sherehe za kuhitimu darasa la saba siku za hivi karibuni na kupelekea kifo chake baada ya jitihada za matibabu na maombi kushindikana.
Baba mzazi wa mtoto huyo,Benjamin Makelo katika maziko hayo alishindwa kujizuia baada ya kushindwa kusimama akisaidiwa na ndugu kumuinua katika kaburi hilo la mwanae.
Raphael Mtafya kiongozi wa mtaa na mwimbaji wa kwaya katika kanisa alilokuwa akisali marehemu huyo,alisema kifo hicho kimejawa na mshangao mkubwa kutokana na kudonolewa na kuku usiku wa saa nane.
Alisema alipotoka kupokea zawadi kwenye sherehe hizo za kuhitimu darasa la saba usiku wakati amelele aliota ndoto kuwa amedonolewa na kuku aliposhituka alimueleza baba yake juu ya ndoto hiyo.
Alisema siku iliyofuata saa saba usiku alishituka kitandani baada ya kuku aliyemuota kumjia na kumdonoa katika paji la uso na ilipofika asubuhi alianza kuugulia maumivu makali.
Alisema baada ya maumivu hayo kuzidi alipelekwa hospitali ya wilaya iliyopo Vwawa na kufanyiwa vipimo ambavyo havikuonesha ugonjwa na ndipo walipo mpeleka kanisani kufanyiwa maombezi.
Mtafya ambaye pia ni barozi wa nyumba kumi katika mtaa huo,aliendelea kusema kuwa baada ya homa kuzidi wakampeleka hospitali ya Rufaa mkoani Songwe ambako nako vipimo havikuonesha ugonjwa.
Alisema baada ya hapo marehemu alirejeshwa nyumbani na alizidi kuumia huku jicho moja likiziba na alianza kuharisha mfurulizo na ilipofika usiku wa saa nane ya kuamkia jana alifariki dunia na amezikwa leo.
’Mimi ni shemansi wa kanisa na ni barozi wa mtaa shina namba 2,baba wa mtoto ni Mwalimu wa sande,mtoto alikuwa mwimbaji na mwenye kuijua vyema bibiria,tulijaribu kumuombea lakini ilishindi kana,kifo chake kimewashangaza wengi’alisema Mtafya.
Mwenyekiti wa mtaa wa mtaa wa Maejengo Leonard Mwambene alisema ameshiriki maziko hayo huku akijiuliza chanzo cha kifo hicho na kuwa yote hayo ni mipango ya mungu.
Alise
Afisa mtendaji wa kata ya Hasanga Frola Ndamu licha ya kukiri kuwepo na tukio hilo,alisema hizo ni kazi za mungu kwani akipa ngacho hakuna binadamu anayeweza kuzuia.
Kamanda wa polisi mkoani Songwe Augostino Senga,alisema suala hilo halijafika mezani kwake,lakini kuku wanasumu nyingi,ikiwa mtoto alidonolewa alafu wakamchelewesha kumchoma sindano ya tetenasi inaweza sababisha kifo.






Comments
Post a Comment