MTOTO WA MIAKA 12 AFARIKI DUNIA AKIDAIWA KUDONOLEWA NA KUKU TETEA,IMANI ZA KISHIRIKINA ZATAJWA.
Na Ibrahim Yassin, Mbozi.
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida mwanafunzi wa darasa la saba aliyehitimu siku za hivi karibuni,Josiah Mwambene (12) amefariki Dunia akidaiwa kudonolewa na kuku tetea kwenye paji la uso akitokea kupokea Zawadi kwenye sherehe (Mahafali ).
Baba mzazi wa mtoto huyo,Benjamin Makelo alipotakiwa kuelezea sababu ya kifo cha mwanae hakuweza kuhimili kuzungumza akibubujikwa na machozi huku akisema kifo cha mwanae ni bepo.
Baadhi ya wakazi wa eneo hilo wakiongozwa na Deo Mkondya wamelihusisha tukio hilo na Imani za kishirikina kutokana na mazingira yalivyo ya kuku kumdonoa mwanadamu na kusababisha kifo.
Akizungumza leo mwezi Oktoba 12/2025 ndugu wa karibu na mtoto huyo Raphaer Mtafya alisema Josiah alikuwa ni akili kubwa darasani,siku ya sherehe za kuhitimu darasa la saba zilizofanyika mwezi uliopita alipata Zawadi nyingi kwa ufauru wa masomo na kujibu vyema maswali ikiwemo kuwataja Marais wa afrika.
Alisema baada ya kupokea zawadi hizo alirejea nyumbani akiwa kitandani amelala usiku was aa nane alivamiwa na kuku tete ana kumshambulia usoni baada ya kujiokoa alimueleza baba yake kilichotokea na ilipofika asubuhi walimpeleka kwenye maombi.
Alisema baada ya maombi kesho yake alijisikia vibaya ndipo alipopelekwa hospitalini Vwawa kwa ajili ya uchunguzi ambapo vipimo havikuonesha ugonjwa na kesho yake walimpeleka hospitali ya Rufaa jijini Mbeya ambako nako vipimo havikuonesha ugonjwa.
Anasema baada ya hapo walizidi kumuombea kanisani huku jicho likiwa limevimba na kuziba akaanza kuharisha mfurullizo ambapo walimvalisha pampasi mithiri ya mtoto mchanga, ilipofika usiku wa saa 9 kuamkia leo,alifariki dunia.
‘’Mimi ni shemansi wa kanisa nani barozi wa mtaa shina namba 2,baba wa mtoto ni Mwalimu wa sande,mtoto alikuwa mwimbaji na mwenye kuijua vyema bibiria,tulijaribu kumuombea lakini ilishindikana,kifo chake kimewashangaza wengi’alisema Mtafya.
Mwenyekiti wa mtaa wa mtaa wa Maejengo Leonard Mwambene alisema alipigiwa simu na msaidizi wake kumueleza hali ilivyotokea kuhusu kifo na kuwa walimueleza alivamiwa na kuku mwezi uliopita na jinsi alivyopatiwa matibabu ambapo jana usiku alifariki dunia.
Alisema tukio hilo ni la kusikitisha na halijawahi kutokea katika mtaa wake,akishangazwa kuku ambaye hana vifaranga kusababisha kifo cha mtu huku akiwaasa wazazi kutojichanganya Pamo ja na mifugo ili kuhepuka na hatari kama hii iliyojitokeza kwa mtoto Josiah.
Afisa mtendaji wa kata ya Hasanga Frola Ndamu licha ya kukiri kuwepo na tukio hilo,alisema alipigiwa simu kufahamishwa uwepo wa msiba ila mwanzo wa tukio na sababu ya kifo hakuelezwa.
Alisema mambo ya vifo yana sababu nyingi, inawezekana mtoto alikuwa na maradhi mengi ne,kuvamiwa na kuku ikatajwa kuwa ni sababu ya kifo,yote kwa yote mungu muumba mbingu na ardhi ndiye anayejua.
Kamanda wa polisi mkoani Songwe Augostino Senga,alisema suala hilo halijafika mezani kwake,lakini kuku wanasumu nyingi,ikiwa mtoto alidonolewa alafu wakamchelewesha kumchoma sindano ya tetenasi inaweza sababisha kifo.

Comments
Post a Comment