Miradi ya Bil,20.5 kutembelewa na Mwenge mkoani Rukwa
Na Ibrahim Yassin. Songwe.
Mwenge wa uhuru kukagua miradi 43 yenye thamani ya Bilioni 20.5 katika wilaya 4 Halmashauri 5 mkoani Songwe.
Mwenge huo wa uhuru umepokelewa leo Octoba 2/2025 katika kijiji na kata ya chitete wilayani Momba mkoani hapa ukitokea mkoani Rukwa.
Akikabidhi mwenge huo kwa mkuu wa mkoa wa Songwe, mkuu wa mkoa wa Rukwa Charles Makongoro Nyerere amesema mwenge huo ulikagua miradi ambayo yote imepokelewa.
Nyerere amesema katika wilaya zote nne za mkoa wa Rukwa mwenge huo ulikagua miradi yenye thamani ya zaidi ya Bilioni 55 ambayo ilikaguliwa na mingine iliwekewa mawe ya msingi.
Amesema mwenge huo ulio asisiwa na wazee baba wa Taifa Hayati mwalimu Julias Nyerere na Hayati Abeid Aman Karume lengo kuu ni kumulika penye kiza kuleta upendo na utulivu penye chuki.
Akiupokea mwenge huo, mkuu wa mkoa wa Songwe Jabir Omary Makame amesema mwaka 2024 mwenge huo ulikagua miradi 46 yenye thamani ya Bilioni 18 lakini mwaka huu 2025 mwenge huo utakaguq miradi 43 yenye thamani ya Bilioni 20.8.
Amesema miradi hiyo ipo katika wilaya nne Halmashauri 5 za mkoa wa Songwe huku akitarajia zoezi kwenda vizuri.
Amesema serikari ya awamu ya sita ilifanya kazi kubwa ambapo fedha zaidi ya Bilioni 7013 zilitolewa kujenga miradi ya maendele na kuufanya mkoa huo kung'ara .
Ameongeza kuwa mkoa wa Songwe ni lango la nchi za kusini mwa Afrika (Sadc) hivyo wao kama viongozi wameisimamia ipasavyo Ilani ya Chama cha Mapinduzi chini ya mwenyekiti Dkt,Samia Suluhu.
Hata hivyo mkuu huyo wa mkoa baada ya mazungumzo hayo aliukabidhi mwenge huo kwa mkuu wa wilaya ya Momba Elias Mwandobo ambaye anaendelea kuukimbiza na kukagua miradi katika kata mbalimbali wilayani humo.
Akizungumza mara baada ya makabidh iano hayo kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Ismail Ally Ussy amesema wameikagua na kuweka mawe ya msingi miradi mkoani Rukwa ambayo imejengwa na kukamilika bila kuwepo na changamoto.
Amesema leo wapo mkoani Songwe kuendelea mbio hizo huku akiomba mambo matatu kwa mkuu wa mkoa ambayo ni Nyaraka sahihi za miradi, vifaa vya kupimia na wataalam wa.miradi hiyo.
" ninamfahamu mkuu wa mkoa makame ,leo ni mara yake ya pili kupokea mwenge huu,mara ya kwanza alipokea akiwa mkuu wa wilaya ya Gairo na sasa anaupokea akiwa mkuu wa mkowa
wa Songwe, naamini tutapata ushirikiano mzuri "amesema Ussy.
Aidha mkimbiza huyo wa mwenge kitaifa amesema serikali ilitoa maagizo kwa wakurugenzi wa halmashauri zote kutumia makusanyo ya mapato ya ndani kujenga ya maendeleo na amejionea jinsi wakurugenzi hao walivyo timiza agizo hilo.
Mwenge huo wa uhuru umepokelewa kwa kishindo kikubwa baada ya wadau nbalimbali kushiriki huku vikundi vya hamasa vikisherehesha mapokezi hayo.





Comments
Post a Comment