WAZEE WAMETAKIWA KUWAJENGA WATOTO WAO ILI WAWE MSAADA KWAO BAADAE

Na Israel Mwaisaka, Nkasi
‎Wazee wametakiwa kuwatengeneza Watoto vizuri kwa kuwajengea mazingira mazuri ya kimaisha Ili waweze kuja kuwa na msaada kwao hapo baadae.
‎Wito huo umetolewa Leo na afisa elimu msingi wilayani Nkasi Eliud Njogela ambaye alimwakilisha mkuu wa wilaya Peter Lijualikali kwenye kikao Cha Baraza la Wazee ambapo amesema Ili kijana awe mzuri baadae Ni lazima aandaliwe vizuri.
‎Hilo lilikuja baada ya mwenyekiti wa Baraza Hilo la Wazee Joshua Mgaya alipogusia hoja ya Wazee kupelekwa kwenye nyumba za malezi za serikali kwa Wazee na kuwa hilo lisipewe kipaumbele Sana Bali tujikite kuwalea Watoto vizuri na kuwajengea mazingira mazuri ya kiuchumi Ili waweze kuja kuwa walezi wa Wazazi wao.
‎Alidai kuwa haitakua rahisi Sana kwa Wazee wote kupelekwa kwenye nyumba za malezi za Wazee na Ni kitu ambacho serikali haiwezi kumudu Bali njia pekee Ni Wazazi kulelewa katika familia zao labda kwa wale Wazee ambao Ni lazima wapelekwe huko kulingana na mazingira waliyonayo.
‎Amefafanua kuwa Kama Watoto wakijengwa vizuri kiuchumi na kimaadili wataweza kuwatunza Wazazi wao bila ya changamoto yoyote.
‎Ameenda mbali zaidi kwa kusema kuwa mtu anapokua mzee anakua Kama Mtoto hivyo anatakiwa kulelewa na familia yake na kuwa kuwapeleka kwenye nyumba za malezi ni kuwatengeneza ukiwa kitu ambacho ni kwenda kinyume na maadili yetu Kama Watanzania.
‎Njogera pia aliwaasa Wazee kutoa Wosia au miongozo mbalimbali ya kifamilia kwa Watoto wao wakiwa bado na Nguvu au kupoteza maisha kwani kufanya hivyo kutawafanya kuwa na famili bora.
‎Alidai kuwa uoga wa Wazee wengi Ni kishindwa kuandika au kutoa Wosia wakiamini kuwa kufanya hivyo ni kujitakia mkosi na kufa kitu ambacho siyo sahihi na kuwa Wazee ambao walifanikiwa kuandika Wosia familia zao hazina migogoro na zinaendelea kustawi Kila siku.
‎Baraza hilo la Wazee ni maandalizi ya siku ya Wazee duniani ambayo ufanyika Oktoba 1 ya Kila mwaka.
‎MwishoNa Israel Mwaisaka, Nkasi

Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa