WANASWA NA SIRAHA ZIKIWA NA RISASI KATIKA MSAKO WA TRA,KAMATI NA JESHI LA POLISI
Na Ibrahim Yassin,Songwe
Katika operesheni iliyofanywa na mamlaka ya mapato Tanzania kwa kushiri kiana na Jeshi la Polisi mkoani Songwe imefanikiwa baada ya kukamata Bastora CZ92 Browning namba A 428007 ,CALIBER 6.35MM ikiwa na Risasi zake 6 ndani ya Magazine,Katika mpaka was Tunduma na Black.
Hata hivyo imeelezwa kuwa bastola hiyo bastola hiyo ilikuwa ikitafutwa baa da ya kuibiwa wilayani Mbozi Mei 13/2025, huku watuhumiwa wakiitelekeza na kukimbia baada ya msako huo.
Vikosi hivyo vikiwa Katika muendelezo wa operesheni pia wakiwa kata ya Majengo Tunduma, walifanikiwa kukamata siraha nyingine aina ya Bastola Retay G19C yenye namba R1YGCMOY501 _2400425 CAL9MM ikiwa na Risasi 150 ambayo ilitelekezwa maeneo hayo na watu ama mtu asiyejulikana.
Mbali na kukamata Bastola hizo, maafisa hao waliendeleza doria iliyofanik isha kukamata watu watatu majina yao yamehifadhiwa wakazi wa kata ya Ikana walikutwa na silaha aina ya Gobole lililotengenezwa kienyeji likiwa na Risasi 3 maeneo ya Tarafa ya Ndalambo wilayani Momba ambapo upelelezi unaendelea.
Aidha katika Opelesheni shirikishi kati ya Maafisa wa TRA na wale wa TISS walifanikiwa kumkamata mtu mmoja jina lake limehifadhiwa katika kituo cha ukaguzi /huduma ya pamoja (OCBP) Tunduma akiwa na dolla 160.000 za Marekani zikiwa katika maungo yake bila kufuata utaratibu wa kisheria.
Mbali na kuzikamata fedha hizo,pia maafisa hao walifanikiwa kukamata noti aina ya kwacha zinazodhaniwa kuwa bandia kutoka nchini Zambia zikiingizwa nchini ambapo mtuhumiwa alikamatwa na kesi yake ipo mahakamani.
Namba za noti hizo ni FA 126314129 zipo noti 14,na namba FA 125184266 zipo noti 15 , namba EH 122082951 zipo noti 13 ,namba EH 122083003 zipo 10 ,namba EH 122082339 zipo 2, namba FA 125184149 zipo 2, na namba EH 122082407 ipo noti 1.
Meneja msaidizi wa Forodha mkoani Songwe, Nsajigwa Mwambegele amesema Operesheni hizo ni endelevu na wamekuwa wakishirikiana na jeshi la polisi lengo kubwa ni kuhakikisha wafanyabiashara wote wanafuata utaratibu uliowekwa.
Amesema kazi yao kama TRA ni kukusanya mapato, hivyo wanalazimika kufanya doria kuwabana wanaovusha bidhaa kwa njia za vipenyo huku wakifanikiwa kukamata bidhaa nyingi.
"Tumekuwa tukitoa elimu kwa wafanyabiashara kupitia jumuiya zao wengi wamekuwa wakilipa mapato vizuri hali iliyopelekea wavuke lengo la ukusan yaji japo wapo wanaopitisha bidhaa kwa njia hizo lakini tutawabaini ni Vem a wakaacha "amesema Mwambegele.
Kamanda wa polisi mkoani Songwe Augostino Senga amesema hawatata lala kwani wamejipanga kuhakikisha wanadhibiti vitendo vya uhalifu na kuwataka wanaodhani Songwe ni kimbilio la uharifu waache mara moja.
Amesema operesheni shirikishi walizofanya na TRA wamefanikiwa kukamata bidhaa nyingi ikiwemo silaha na noti bandia hivyo wataendelea na doria za mara kwa mara kuhakikisha mkoa unaendelea kuwa salama.






Comments
Post a Comment