Wanafunzi sekondari ya SUMAGHA Tunduma wachekelea darasa la Sayansi
"Miaka ya nyuma tulikuwa tunayaogopa masomo ya Sayansi, lakini kwa sasa tunayapenda kutokana na ujion wa vifaa vya kisasa tunasoma kwa vitendo darasa zima tunapata Divishen One "
Na Ibrahim Yassin,Songwe
Wanafunzi wa shule ya sekondari SUMAGHA iliyopo kata ya Mpemba halmashauri ya mji Tunduma mkoani Songwe wameeleza namna wanavyo yapenda masomo ya Sayansi kutokana na uongozi wa shule hiyo kuwawekea vifaa vya kisasa na wanasoma kwa vitendo.
Shule ya SUMAGHA iliyoanzishwa Januari 27/2016 yenye usajili namba S 5538 imeingia kwenye nafasi ya kumi bora kitaifa kutokana na kufaurisha Wanafunzi darasa zima na kufanikiwa kuitokomeza alama 4 na O.
Wakizungumza na Dira kamilifu baada ya kufika shuleni hapo wanafunzi hao wamesema wanajiona fahari kusoma katika shule hiyo kutokana na uwepo wa miundombinu rafiki na walimu wenye uwezo mkubwa was kufundisha.
James Emmanuel mwanafunzi aliyehitimu kidato cha 4 mwaka jana na mkazi wa jijini Mbeya amesema wakatati anahamia shuleni hapo akitokea moja ya shule iliyopo Mbeya alikuwa na uwezo mdogo darasani lakini walimu walimpatia Program maalum.
Amesema baada ya miezi 3 ya Program hiyo katika masomo ya Sayansi aliweza kuendana na wanafunzi aliowakuta na katika mitihani ya kuhitimu kidato cha 4 alifanikiwa kupata Divishen One ya 7.
Nae Annastazia Kirumbo mwanafunzi aliyehitimu kidato cha 4 na kupata alama B ya ufaulu amesema amepata kuwawekea katika shule aliyopo sasa akiwa kidato cha 5 na kuwa wakatati anasoma SUMAGHA alikuwa na uhakika wa kufanya vizuri kutokana na weredi wa ufundishaji wa walimu wa masomo hayo.
Amesema Mbali na shule hiyo kufaulisha kwa kiwango cha juu masomo ya Sayansi pia wanafunzi wote wanaofanya mitihani ya kuhitimu kidato cha 4 kila mwaka wanachaguliwa darasa zima kujiunga na masomo ya kidato cha 5.
Mwl, Erasto Kabuje wa somo la Chemistry amesema uwepo wa vifaa vyote vya kusoma kwa vitendo masomo ya Sayansi kumeleta mapinduzi makubwa kwa wanafunzi kuyapenda masomo na Miaka 5 mfurulizo darasa zima wanachaguliwa kujiunga kidato cha 5 tena kwa ufaulu wa juu.
" wakati nakuja kufanya kazi shuleni hapa wanafunzi wengi walikuwa wanaogopa kusoma Sayansi wakiwa na imani kuwa masomo ni magumu,lakini baada ya Miaka 3 nyuma kufauru darasa zima wa meanza kuyapenda masomo hayo amesema Mwl, Kabuje.
Mkuu wa shule hiyo, Mwl, Evodius Kapela amesema wanafunzi wanahaki ya kufurahia masomo ya Sayansi kwani darasa lao limesheheni vifaa vya kisasa, wamekuwa wakisoma kwa vitendo na wamekuwa wakifanya vizuri kwenye mitihani ya Taifa.
Amesema kazi kubwa waliyonayo ni kuwapeleka wanafunzi hao kwenye ziara za kimasomo ndani na nje ya mkoa wa Songwe,na kwa Miaka 5 mfurulizo shule hiyo Imefaulisha wanafunzi darasa zima na wamefanikiwa kuitokomeza alama 4 na O.
Amesema shule hiyo inaeneo la hekari 15.5 yapo madarasa na mabweni ya kutokana kwa wanafunzi wa jinsia zote huku kukiwa na ulinzi wa kutosha na maadili mazuri kwa dini zote wakiwa na duka last shule lenye mahitaji yote muhimu.
Amesema kwa miaka 6 mfurulizo mitihani ya Necta wanafunzi darasa zima wanachaguliwa kujiunga kidato cha 5 kwani mwaka 2022 wanafunzi waliofanya mitihani ya kidato cha 4 walikuwa 102 wanafunzi 27 walimpata division One wanafunzi 43 Divishen Two na wanafunzi 23 division Three hukukuwa na alama 4 wala 0.
Amesema mwaka 2023 waliofanya mitihani walikuwa 82 kati ya hao 27 walipata One ,37 walipata Two na 11walipata Three na mwaka 2024 waliofanya mitihani kuhitimu kidato cha 4 walikuwa 93 kati ya hao 23 walipata divisheni One, 49 walipata Two na 30 walipata Three hakuna 4 wala 0.
Amesema kwa sasa wanapokea wanafunzi wanaojiandaa kusoma kidato cha Kwanzaa kusoma (pree form one) na kuwa wazazi na walezi wanaohitaji kuwaleta watoto wao wapige simu namba 0745437195 .





Comments
Post a Comment