WACHIMBAJI WATAKIWA KUZINGATIA USALAMA WAO MIGODINI.




Na Ibrahim Yassin.Songwe

Wachimbaji wadogo wa madini ya dhahahu wa vijiji na kata ya Saza wilayani Songwe mkoani hapa wametakiwa kuzingatia usalma wao migodini ili kuhepuka maafa yasiyo ya lazima.

Asilimia 70 ya vijana wa eneo hilo wanaendesha maisha yao ya kila siku kwa kutegemea kazi ya uchimbaji madini, hivyo ili kuimarisha usalama wao wametakiwa kuchukua tahadhari wawapo kwenye mashimo.

Elimu hiyo imetolewa Septemba 06, 2025 na Mkuu wa Kituo cha Polisi Mkwajun i, Mrakibu wa Polisi (SP) Johanes Bitegeko, pamoja na Mkuu wa Kituo cha Polisi Saza, Mkaguzi wa Polisi Mussa Masumbuko, huku wakiwahimiza wananchi na wachimbaji hao kuchukua tahadhari katika maeneo hayo.

Ameaema kulinda afya ni muhimu katika uwajibikaji wa shughuri balimbali kuhepuka madhara kwani maisha yanathamani kubwa kuliko madini.

" Kazi za uchimbaji madini inawaingizia kipato lakini ni muhimu kuchukua tahadhari  kuhepuka maafa"amesema afande Bitegeko.




SP Bitegeko, alisisitiza umuhimu wa kuwepo kwa vifaa kinga wakati wa shughuli za kusaga mawe ya dhahabu kwenye makarasha, huku akieleza kuwa kemikali zinazotumika na vumbi zito linalotokana na shughuli hizo lina madhara makubwa kwa afya.

 Amesema ni  muhimu kwa wachimbaji kutumia vifaa kinga kama barakoa, glovus, miwani na mavazi ya kujikinga ili kupunguza athari hizo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Kituo cha Polisi Saza Mkaguzi wa Polisi Mussa Masumbuko, alitumia nafasi hiyo kuwaelimisha wachimbaji hao, kuhusu umuhimu wa kuweka kumbukumbu za taarifa binafsi kwa wafanyakazi, hususani wanapojihusisha na kazi zinazowapeleka mbali na familia au marafiki wa karibu.

 alifafanua kuwa kuwepo kwa taarifa hizo kunarahisisha upatikanaji wa msaada wa haraka kwasababu taarifa sahihi zitakuwepo na endapo mtu atakumbwa na changamoto au kutoweka ghafla ataweza  kupatikana kirahisi.

Aidha, Mkaguzi Mussa, aliwahimiza wananchi kuwa na utaratibu wa kutoa taarifa mapema wanapotoka maeneo yao, hasa wale wanaokwenda kwenye shughuli za migodini ili kuongeza ufanisi katika kulinda usalama wao na wa wengine.


Baada ya elimu hiyo, wachimbaji na wananchi wa kijiji hicho walitoa shukrani zao za dhati kwa Jeshi la Polisi kwa kujali usalama wao, na waliahidi kuyatekeleza kwa vitendo maelekezo yote waliyopewa, huku wakisisitiza kuwa usalama wao sasa umepewa kipaumbele zaidi.

Kutokana na umuhimu huo wa shughuri za migodini ipo haja kasi ya utoaji elimu kutolewa mara kwa mara kulinda afya na maafa kwa wachimbaji.




Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa