TRA ,KAMATI YA USALAMA WAKAMATA DAWA ZA KULEVYA ZA MAMILIOMI YA FEDHA KTK OPERESHENI ZAK




Na Ibrahim Yassin, Songwe.

Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) mkoani Songwe kwa kushirikiana na Akamati za usalama za wilaya za Momba na Ileje ikiwemo ya mkoa zimefanikiwa kukamata dawa za kulevya za mamiliomi ya fedha.

Lengo la mamlaka hiyo kuendesha operesheni hizo ni kuhakikisha wanadhibiti uingizwaji dawa za kulevya kutoka nchi  za Malawi na Zambia.




Wilaya ya Ileje nchini Tanzania imepakana vijiji vilivyopo Chitipa nchini Malawi ambavyo ni maarufu kilima bangi.

Mji wa tunduma nchini Tanzania umepakana na miji ya Nakonde nchini Zambia ambayo bidhaa nyingi uingizwa nchini kwa njia za panya ikiwemo milungi.

Ujirani wa miji hiyo umepelekea baadhi ya wafanyabiashar a wakishirikiana na wenyeji wa waishio pembezoni mwa mipaka hiyo kubuni njia za vipenyo kupitishia dawa hizo za kulevya.

Upande wa Ileje wanatumia njia ya kuweka madaraja ya miti na mianzi maeneo yaliyo mbali na makazi ya watu kuvushia bidhaa hizo kuja nchini.

Watu wanaofanya biashara hizio wamelazimika kuununua redio,Tv, Sabufa, Sora na bidhaa zingine wanazipeleka Malawi kwenye vijiji ikiwemo kijiji cha Chikutu wakitumia njia hizo kubadilishana vyombo hivyo na Bangi.

Hadi sasa njia hizo za vipenyo zimefika 300 kwa wikaya zote mbili hali iliyoumiza vichwa maafisa wa TRA na Kamati ya usalama na kuunda vikosi kazi kuendesha msako ulioleta mafanikio.


Akizungunza na Dira Kamilifu ofisini  kwake meneja msaidizi wa Forodha mkoani Songwe Nsajigwa Mwambegele amesema waliamua kushirikiana na kamati za usalama kufanikisha opelesheni hiyo.

Amesema vikosi kazi vilivyoundwa vimefanya kazi kubwa kwani bidhaa nyingi Zimekamatwa zikiwemo dawa za kulevya.

Amesema katika operesheni hizo wamebaini uwepo wa njia zaidi ya 300  za panya zinazotumika kuvushia mizigo hiyo.



Amesema hadi sasa wamefanikiwa kukamata bidhaa nyingi na kudhibiti nyia hizo za vipenyo na kuwa zoezi bado linaendelea.

Kamanda wa polisi mkoani Songwe Augostino Senga amesema jeshi lake limejipanga kuhakikisha linadhibiti uingizwaji wa magendo nchini zikiwemo dawa za kulevya.
 
Amesema njia zote za vipenyo zimedhibitiwa na watabaibi na kudhibiti endapo watu hao watabuni mbinu mpya lengo ni kutaka wananchi waendelee kuwa salama.


Ameongeza kuwa utumiaji wa dawa za kulevya zinaharibu nguvu kazi ya vijana ndiyo maana serikali inapiga vita uingizwaji wa dawa hizo nchini na wao kama jeshi la polisi watahakisha wanafanya operesheni za mara kwa mara kuhakikisha  watu wanaokamatwa na bidhaa hizo wanapelekwa mahakamani.

Kuna kila sababu ya kupongeza operesheni hizo
kwani matumizi ya dawa za kulevya yanaharibu maisha ya vijana ambao ni Taifa la kesho.




Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa