TII SHERIA TUJENGE AMANI NA MAENDELEO KATIKA JAMII YETU
Na Ibrahimu Yassin,Songwe
Wananchi wa kitongoji cha Msogezo kilichopo katika kata ya Chitete, wilaya ya Mbozi mkoani Songwe, wametakiwa kutambua na kuzingatia wajibu wao wa kutii sheria za nchi ili kudumisha amani, usalama na maendeleo ya kijamii.
Wito huo umetolewa Agosti 12, 2025 na Polisi kata ya Chitete Mkaguzi wa Polisi Makubi Lagae alipokuwa anatoa elimu ya umuhimu wa kutii sheria kwa wananchi wa eneo hilo ili jamii iendelee kuwa salama.
"Changamoto nyingi za kiusalama na migogoro katika jamii zinatokana na wananchi kutokujua au kupuuza sheria zinazowaongoza, hali inayochangia uvunjifu wa amani na kudhoofisha jitihada za maendeleo, basi kila mwananchi ana wajibu wa kushiriki katika kuimarisha usalama kwa kutoa ushirikiano kwa Jeahi la Polisi, ikiwa ni pamoja na kujiepusha na vitendo vya kihalifu au vya kuchochea vurugu" alisema Mkaguzi Makubi.
Mwisho, wananchi waliopata elimu hiyo walipata fursa ya kuuliza maswali na kutoa maoni juu ya changamoto zinazowakabili, huku wakiahidi kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuhakikisha kuwa sheria na taratibu zinafuatwa.


Comments
Post a Comment