POLISI,WANAHABARI USO KWA USO NA TUME KUJADIRI HAKI ZA BINADAMU KUELEKEA UCHAGUZI MKUU.
Na Ibrahim Yassin,Songwe
Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali na jeshi la polisi mkoani Songwe, wamekutanishwa na maafisa wa Tume ya haki za binadamu na utawala bora kujadili masuala mbalimbali kuelekea uchaguzi mkuu.
Miungoni mwa masuala yaliyojadiliwa umuhimu wa kuandika habari kwa kufuata kanuni na sheria zilizopo pasipo kupendelea chama chochote cha siasa ili kuhepuka taharuki zitakazoweza kuleta machafuko.
Imeelezwa Kuwa mandishi wa habari anahaki ya kuchagua mgombea anaye mtaka na pia anatakiwa kuandika taarifa sahihi na si kuandika taarifa zinazoweza kuvunja haki za binadamu.
Akizungumza jana mbele ya Waandishi wa habari, Stephen Sitami afisa wa Tume ya haki za binadamu na utawala bora amesema Octobe mwaka huu ni mwa ka wa uchaguzi, hivyo anatarajia wanahabari wataandika habari sahihi bila kupendelea upande mmoja na ndiyo maana wamefika mkoani Songwe kuendesha mjadala huo.
Amesema Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzanian ya mwaka 1977 na Katiba ya Zanziba ya mwaka 1984 ambazo ni sheria mama za haki za binadamu zimeeleza mambo hayo na kupinga ukandamizazi.
Amesema pia sheria ya habari ya mwaka 2016 ina vipa haki vyombo vya habari kukusanya taarifa,na kwa upande was jeshi last polisi na huduma saidizi sura ya 322 inawapa wajibu huo Kikatiba kufanya shughuri zao kwa weredi.
Ameongeza Kuwa kutokana na hali hiyo wananchi, vyombo vya habari na vyama vya siasa vina uhuru au haki ya kutoa maoni,kuchaguliwa au kuch agua kiongozi mwenye sifa pamoja na uhuru wa kukusanyika kushiriki mikutano.
Hata hivyo kiongozi huyo, alieleza Kuwa wanahabari wana wajibu wa kueli misha umma juu ya uchaguzi, na kuripoti habari na matukio yote ya uchagu zi kwa usahihi bila upendeleo wa chama au mgombea.
Nae Peter Dihoko afisa wa Tume ya haki za binadamu na utawala bora amesema umakini wa kuripoti taarifa za uchaguzi unatakiwa kwani ziandikwapo taarifa za upotoshaji zinaweza kuleta madhara na watu kuchukiana.
Ameyataja madhara hayo Kuwa ni kuchanganya umma juu ya uwepo wa taarifa zenye utata, kuvuruga maamuzi,kuchochea migogoro, kupoteza imani na jambo furani, kuharibu heshima ya mtu na athari za kiuchumi.
Katakana na hali hiyo amesema waandishi wa habari wananafasi kubwa kwa Jamii ya kuelimisha na kuandika habari za ukweli kutumia karamu zao hali inayoweza kupinga usawa na kulinda amani iliyopo.
Zephania Mzava afisa uchaguzi wa jimbo la Mbozi na Vwawa amesema amefarijika na ujio wa maafisa hao wa haki za binadamu kwani elimu na mijadala iliyofanyika imewapa mwanga mkubwa huku akiwataka wanaha bari kufika kwenye ofisi zao kuuliza kama kuna jambo wanataka kulipatia ufumbuzi.
WASEMAVYO WANAHABARI
Baraka Messa katibu wa chama cha waandishi wa habari mkoani Songwe (Songwe Press Club) amesema wanahabari wamekuwa wakifuata taratibu zilizopo na mambo yote muhimu wameyachukua na huahidi kuyatekeleza huku akiomba waheshimiwe.
Amesema heshima aliyoitaka ni kuhakikisha wanahabari wanapewa magari mazuri kuhepuka ajari na wawe wanaongozana na viongozi ili kuwahi picha na matukio badala ya gari wanazopnda kuwa mwishoni Katika misafara.
Nae Moses Ng'wat mwandishishi kutoka kampuni ya Business Time ames ema yote yaliyosemwa na kujadiliwa watayafanyia kazi kama wanahabari na pia alisisitiza na kuahidi kuandika taarifa za uchaguzi kwa weredi pasipo shaka.
Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa Habari mkoani Songwe Stephano Simbeye licha ya kupongeza muenendo wa mjadala huo, amesema waand ishi wa habari wengi wanawajibika kwenye vyombo vyao wanavyo fanyia kazi na huko wanapata elimu kama hiyo.
Amesema shiva kubwa iliyopo ni baadhi wa watu wenye simu za smatph one wamekuwa wakiripoti matukio bila kujari kuwa litapokelewa visit na walaji kisha wanazirusha mitandaoni kupitia simu zao.
Amesema kutokana na hali hiyo ya kila mwananchi mwenye simu ya smatp hone anasambaza taarifa na kuleta taharuki inachukuliwa kuwa ni waand ishi wa habari,hivyo aliomba mamlaka husika ziongeze udhibiti kwa watu hao.
MKUU WA POLISI MKOA AELEZA UMUHIMU WA MAFUNZO.
Baada ya mafunzo hayo, Kamanda wa polisi mkoani Songwe Augustino Senga akizungumza kwaniaba ya jeshi hilo amesema mafunzo hayo yatawao ngezea weredi katika kulinda raia kuelekea uchaguzi mkuu.
"Kimsingi mafunzo haya yanatukumbusha kulinda na kuheshimu haki za binadamu na jinsi ambavyo tunaweza kutekeleza sheria katika mazingira yaliyo salama na kutimiza majukumu yetu kwa kuzingatia sharia za nchi” amesema Kamanda Senga.
Varrey Kwembe kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Songwe amesema amefarijika kuona mjadala kuwa mzuri na kuhusu suala la wanahabari gari Lao kuwa mwisho wakati wa misafara ya viongozi ni kweli hali hiyo amesema inawachelewesha kupata matukio.
Amesema masuala yote yaliyojadiliwa likiwemo hilo la wanahabari atal ifikisha ofisini kwa ajili ya kufanyiwa kazi huku akiwasisitiza wanahabari kuyazingatia yote yaliyojadiliwa kwani wao wanamchango mkubwa wa kuelimisha jamii.
KAZI YA TUME NA KUANZISHWA KWAKE
Tume ya haki za binadamu na utawala bora ilianzishwa kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 sura ya 6 ibara 6 ibara ya 129_131 na sheria ya tume ya haki za binadamu na utawala bora sura ya 391.
Moja ya kazi zake zimeainishwa katika kifungu cha B (1) cha sheria hiyo ni kupokea malalamiko yanayohusu uvunjwaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora na kuifanyia uchunguzi.
Miungoni mwa malalamiko yanayoweza kujitokeza ni mwenendo wa mtu ama watu au taasisi yeyote katika kutekeleza madaraka au utekelezaji unaokiuka madaraka.
Kazi nyingine ni kuchunguza matumizi au matendo ya watu wenye madaraka katika utumishi wa serikali kuu,serikali za mitaa,halmashauri za wilaya,miji, manispaa na zinginezo.
MAANA YA DHANA MUHIMU.
MTAWALA
Ni mtu aliyeaminiwa na kupewa dhamana ya matumizi ya mamlaka kisiasa, kiuchumi au vinginevyo katika kusimamia rasilimali za umma,pia ni mtu aliyepewa dhamana ya kufanya maamuzi ya kimamlaka kwa faida ya jamii.
Utawala (Governence) unaweza kuelezwa kuwa ni matumizi ya mamlaka kisiasa,kiuchumi au vinginevyo katika kusimamia rasilimali za Taifa, vile vile utawala ni mpango wa kufanya maamuzi ya kimamlaka kwa faida ya rasilimali za umma.
UTAWALA BORA.
Utawala bora ni zoezi la wenye madaraka katika maamuzi kuamua ni namna gani rasilimali za Taifa zitumike ya kuboresha maisha ya wananchi, mfumo ambazo unaendelea kwamba utawala bora unataka jamii iendeshe mambo yake kwa kufuata misingi ya uwazi kwa matakwa ya wengi.
MISINGI YA UTAWALA BORA..
Misingi ya utawala bora imejengwa na ushirikishwaji (Participatio n) ,Maridhiano (Concensus Orientation) ,Mwitikio (Responsivenes s) ,Matokeo bora na ufanisi ( Effectiveness and Efficiency).
Uwajibikaji (Accountability),Uwazi (Transparency) ,Usawa (Equity) ,Utawala wa sheria (Rule of Law) , Maono ya kimkakati (Strategic Vision) na Uadirifu (Integrity).
NGUZO ZA UTAWALA BORA.
Dhana ya utawala bora ni dhana ambayo inatokana na nguzo mbalimbali za utawala ambazo zimekuwepo duniani tangu kuanza kwa ustaarabu ambapo zipo nguzo sita.
Nguzo ya kwanza ni katiba ya Kidemokrasia yenye ridhaa ya wananchi (Democratic Constitution) ,Kulinda, kukuza na kuheshimu haki za binadamu ( Protection, promotion and respect for human rights).
Utawala wa sheria (Rule of Law) ,mgawanyo wa madaraka ((Separation of power), Uhuru wa mahakama (Independence of the judiciary) na Uhuru wa habari na uhuru wa vyombo vya habari (Freedom of expression and the freedom of the press.
UMUHIMU WA UTAWALA BORA.
Katika nguzo yeyote ile ya uongozi kuanzia kitongoji, kijiji,halmashauri hadi ngazi za kitaifa,utawala bora ni muhimu na unasaidia mambo yafuatayo.
.Matumizi mazuri ya rasilimali za nchini,.Maendeleo endelevu. Kupungua kwa umasikini, ujinga na maradhi. Kutokomea Kwa rushwa. huduma bora za jamii.Amani na utulivu na kuheshimiwa kwa haki za binadamu.na utatuzi wa migogoro kwa mujibu sheria na utaratibu.
ATHARI ZA UKIUKWAJI WA MISINGI YA UTAWALA BORA.
Matumizi mabaya ya rasilimali za nchi kuongezeka kwa umasikini,ujinga na maradhi.Kuongezeka kwa rushwa. huduma mbovu za jamii. Kuhatarisha amani na utulivu. Kutoheshimiwa kwa haki za binadamu kuongezeka kwa dhuruma na uonevu.
CHANGAMOTO ZA UTAWALA BORA.
Changamoto za utawala bora ni nyingi katika uendeshaji wa sekta za umma hapa nchini,baadhi yake ni......
RUSHWA.
Pamoja na hatua na mikakati mbalimbali kuundwa ili kukabiri suala la rushwa, tatizo hili limepungua kwa kiwango kidogo, hivyo mikakati madhubuti zaidi inahitajika kukabiliana na tatizo hili na kulifuta kabisa kwenye jamii.
KUKOSEKANA KWA USHIRIKI NA USHIRIKISHWAJI.
Viongozi kushirikisha jamii na wadau katika miradi na shughuri za maendeleo kunasababisha utawala bora kutotekelezeka kwa urahisi katika ngazi mbalimbali.
Mwisho.







Comments
Post a Comment