POLISI SONGWE YAPATA MAGARI 6 MAPYA KUENDELEA KUKABILIANA NA UHALIFU



Na Ibrahimu Yassin,Songwe

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Augustino Senga Septemba 08, 2025 amekabidhi jumla ya magari 6 mapya kwa ajili ya kuimarisha utendaji kazi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe, hususan katika kuzuia na kupambana na uhalifu.

Magari yaliyokabidhiwa ni pamoja na Toyota Land Cruiser Hardtop 5D, mawili ambayo yametolewa kwa matumizi ya Mkuu wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Songwe pamoja na Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) Mkoa wa Songwe, huku Magari 3 aina ya Toyota Hilux Double Cabin yametolewa kwa ajili ya wakuu wa upelelezi wa makosa ya jinai katika Wilaya ya Mbozi, Momba na Songwe ikiwa ni pamoja na gari moja aina ya Land Cruiser GXR 300 Series kwa matumizi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe.


Akizungumza wakati wa hafla hiyo fupi ya makabidhiano, Kamanda Senga aliwataka madereva wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe kuyatunza magari hayo kwa uangalifu mkubwa ili yaweze kuwa kwenye hali nzuri na kutumika kwa muda mrefu, huku akisisitiza kuwa, utunzaji mzuri wa rasilimali hizo utawezesha Jeshi la Polisi kuendelea kuaminiwa na kupata magari mengine kwa wakati ujao kwa manufaa ya Jeshi na taifa kwa ujumla.

Vilevile, Kamanda Senga alitumia nafasi hiyo kumshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutoa magari hayo kupitia kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Camillus Wambura, huku akiahidi kuwa magari hayo yatatumika ipasavyo katika kuhakikisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao Mkoa wa Songwe.


Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa