OPARESHENI YA TRA KAMATI YA USALAMA WAFANIKIWA KUKAMATA MAGENDO TOKA ZAMBIA NA MALAWI.
Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Kwa kushirikiana na kanati ya usalama wamefanikiwa kukamata bidhaa za magendo kupitia opelesheni endelevu.
Katika opelesheni hiyo zilifanyika katika mipaka ya ileje na malawi na Tunduma na zambia.
Mipaka hiyo ya Malawi na Tanzania na Zambia imetajwa kuwa na njia 300 za vipenyo vilivyopo mwambao wa mto Songwe na maeneo ya Tunduma hadi Momba.
Miungoni mwa bidhaa zilizo kamatwa ni Vipodozi aina mbalimbali .mafuta ya taa.mafuta ya kula.Pombe kali na bidhaa zinginezo kutoka nchi ya Zambia na malawi.
Akizungumza jana na Dira Kamilifu. Meneja msaidizi wa forodha mkoa wa Songwe Nsajigwa Mwambegele amesema lengo la opelesheni hizo ni kudhibiti uingizwa wa bidhaa za magendo kwa njia za panya.
Amesema bidhaa nyingi zinazoingia ni zile zilizipigwa magufuku kuingia nchini na zingine ni halali ila zinapitishwa bila kulipia kodi.
Amesema vipodozi vilivyokamatwa vinataifishwa na wanawakabidhi maafisa wa chakila na dawa ambao wamekuwa wakiziteketeza kwa kuzichoma moto.
Mwambegele amesema wamewa wakishirikiana na kamati za usalama wilaya ya Ileje na Momba pamoja na kamati ya usalama ya mkoa.
Amesema operesheni hizo zimezaa matunda matunda na kupekekea wangine kuacha kupitisha bidhaa kwa njia za vipenyo na kuamua kulipia na kupita njia halali.
Amesema kutokana na hali hiyo wamefanikiwa kukusanya mapato mengi na kuvuka lengo.
Amesema wamekuwa wakishirikiana vyema na jamii hasa jumuiya za wafanyabiashara kwa kutoa elimu na kushiriki shughuri za kijamii.
Kamanda wa polisi mkoani Songwe Augostino Senga amesema jeshi lake kwa kushirikiana na TRA wamefanikiwa kukamata magari . Pikipiki na bajaji zikibeba vipodozi..vitenge.mafuta na bidhaa nyingine zilizopigwa marufuku kuingia nchini ambazo zinaingizwa kwa njia za vipenyo.
Amesema ghalama za bidhaa hizo hazijulikani kwa kuwa watuhumiwa wengi wanapokimbizwa wanaitelekeza mizigo wao wakikimbilia kisikojulikana na wengine wanakamatwa na kuwajibishwa kwa mujibu wa sheria.
Aidha Kamanda senga amewataka wafanyabiashara kufuata taratibu zilizowekwa ili kuhepuka kukunbwa na mkono wa sheria.





Comments
Post a Comment