KUHITIMU ELIMU YA MSINGI SIO MWISHO WA MASOMO SAFARI BADO INAENDELEA.



Na Ibrahim Yassin..Songwe

Wahitimu wa Shule za Msingi nchini wametakiwa kukaza buti na kujitunza kwani safari yao kielimu bado inaendelea.

Kuhitimu darasa la saba sio mwisho wa elimu hivyo wanayakiwa kijitunza na kujiandaa na elimu ya sekobdary mwakani

Rai hiyo imetolewa leo na Afisa Habari wa Polisi Mkoa wa Songwe, Koplo Issa Mwadangala alipokuwa akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Mahenje wilayani Mbozi mkoani hapa.


Koplo Mwandagala.. amewataka wanafunzi hao kutumia muda wao wa mapumziko kwa kufanya mambo yenye tija, huku akiwasisitiza wanafunzi hao kuwa kipindi ambacho wapo nyumbani au kwa ndugu wanapaswa kuonesha tabia njema ambazo walijifunza shuleni.

"Acheni kujiingiza kwenye vishawishi vinavyoweza kuwapotosha kama matumizi ya dawa za kulevya, kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi katika umri mdogo, pamoja na kujihusisha na michezo haramu ya kamari, kwani mambo hayo yanayoweza kuharibu na kukatisha kabisa ndoto zenu" alisema Koplo Issa.



Aidha, Koplo Mwandagala.. aliwaeleza wanafunzi hao kuwa sehemu ya msaada kwa wazazi na walezi wao ni kushiriki kazi ndogo ndogo za nyumbani kama njia ya kujifunza kuwajibika na kuthamini mchango wa familia katika maisha yao, huku akisisitiza umuhimu wa nidhamu na kuheshimu kila mtu katika jamii wanapokuwa kwenye kipindi cha kusubiri matokeo, kwani huo ndio msingi wa kuwa raia wema na wenye maadili mema.


Katika kuhitimisha, Koplo Issa alieleza kuwa Dawati la habari Mkoa wa Songwe litaendelea kushirikiana na jamii katika kutoa elimu ya kujikinga na uhalifu, hasa kwa watoto na vijana wanaohitimu elimu ya msingi, sekondari, vyuo vya kati na vyuo vikuu, huku akiwaomba wazazi, walimu na viongozi wa maeneo husika kuendelea kuwa karibu na vijana hao ili kuwasaidia kufanya maamuzi sahihi kuelekea maisha ya sekondari na utu uzima.

Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa