KAZUKAMWE AWASHAURI WANANCHI WASIUZE ARDHI KIHOLELA BALI WAITUMIE KUJIENDELEZA KIUCHUMI
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Nkasi Kaskazini Salum Kazukamwe amewataka Wananchi kuitunza vyema rasilimali ardhi waliyonayo na kuacha fikra ya kuiuza kwani itawezesha kukabiliana na umaskini kwa kuanzisha shughuli mbalimbali za uwekezaji.
Ameyasema hayo Jana katika mikutano ya kampeni katika vijiji vya Mkole na Ipanda kata ya Nkomolo ambapo amedai kuwa ardhi Ni moja ya rasilimali muhimu katika kuyafikia maendeleo na kuwa ufike wakati tuachane na mawazo hafifu ya kuuza ardhi Bali tuitumie kuweza kujiendeleza kimaisha.
Amesema kuwa Kama atapata ridhaa ya kuchaguliwa kuwa Mbunge moja Kati ya mambo atakayoyafanya Ni kuipa ardhi thamani Ili wale waliyonayo waweze kunufaika nayo.
Sambamba na Hilo amedai kuwa atakwenda kuhakikisha changamoto ya ukosefu wa maji na ujenzi wa zahanati nzuri katika vijiji hivyo vinapatikana Tena kwa wakati kwani hivyo Ni moja ya vipaumbele vikubwa kwake.
Alidai kuwa Jimbo Hilo la Nkasi Kaskazini awamu iliyopita lilikua likiongozwa na Mbunge kutoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kuwa Sasa ni wakati wa CCM kuweza kuliongoza Jimbo Hilo kwa kufuata sera dhabiti za Chama hicho tawala
Mgombea Udiwani wa kata ya Nkomolo Stephen Tontololo kwa upande wake amewataka Wananchi wampe ridhaa ya kuwa Diwani wa kata hiyo Ili aweze kushirikiana na Mbunge wake Kazukamwe katika kusukuma agenda za maendeleo kwa Wananchi.
Alidai kuwa kata ya Nkomolo inakabiliwa na changamoto nyingi ambazo zinahitaji Diwani makini ambaye ataweza kuzishirikisha changamoto hizo kwa Wadau wengine was maendeleo ikiwemo serikali katika kuona utatuzi was changamoto hizo unapatikana
Katibu wa CCM wa wilaya Nkasi Anastasia Almasi yeye alisisitiza suala la kuchagua mafiga matatu kwa maana ya Rais,Wabunge na Madiwani wote watokanao na chama Cha Mapinduzi Ili kuweka muunganiko mzuri katika kuwatumikia Wananchi
Mwisho

Comments
Post a Comment