JINSI MABILIONI YA RAIS DKT,SAMIA YALIVYOJENGA MIRADI YA ELIMU SONGWE DC
-Wanafunzi sasa wapenda shule baada ya serikali kujenga shule mpya na kuzikarabati chakavu na kuweka miundombinu rafiki.
Na Ibrahim Yassin,Songwe
SERIKALI ya awamu ya sita iliyokuwa chini ya Rais Dkt,Samia Suluhu,i metumia kiasi cha zaidi ya Bilioni 8 kujenga shule mpya na kuzikarabati shule chakavu kwa kipindi cha miaka mine hali iliyoamsha hali ya wana funzi kupenda kusoma na kuongeza ufauru.
Wilaya ya Songwe ni mpya ilimegwa kutoka wilaya ya Chunya mkoani Mbeya miaka kadhaa iliyopita iliyopita huku ikikabiriwa na changamoto nyingi zikiwemo za uhaba wa madarasa na shule mpya kutokana na upya wake.
Mgawanyo wa wilaya hiyo ulipelekea mwenyekiti wa halmashauri hiyo Abraham Sambila,Mbunge wa jimbo hilo Phillipo Mulugo wakishirikiana na wakuu wa wilaya na wakurugenzi pamoja na madiwani kuumiza vichwa kupanga namna ya kuondokana na changamoto hiyo.
Kupitia vikao mbalimbali vya mabaraza ya madiwani viliketi kwa nyakati tofauti kwa kipindi cha miaka minne wakipanga namna ya kuiboresha Songwe katika sekta ya elimu huku mbunge Mulugo akipiga chapuo Bungeni kuomba fedha kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya.
Lengo la kuomba fedha hizo ni kujenga shule jirani na makazi ya watu ili kusogeza huduma kwa wananchi ambapo wakazi wa kata nyingi walikuwa mbali na shule ambapo wanafunzi walilazimika kutembea umbali mrefu kwenda shule na kuhatarisha usalama wao.
Maombi hayo yalizaa matunda ambapo serikali ya awamu ya sita ilisikiliza kilio cha wananchi kupitia Mbunge wao na kutoa kiasi cha Tsh,2,920,12 9,852.29 kujenga shule mpya na kuongeza madarasa katika shule za zamani.
Baada ya ujio wa fedha hizo,mkurugenzi mtendaji na timu yake walila zimika kutuliza akili kwa kuweka mikakati ya matumizi bora na nidhamu ya usimamizi wa fedha hizo hali iliyopelekea miradi kukamilika kwa wakati.
Akizungumzia ujio wa fedha hizo,mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo,Secilia Kavishe,anasema walipokea fedha hizo Tsh,Bilioni 2.920 kutoka serikali kuu na kuanza ujenzi wa miradi kupitia wakandarasi walioshinda dhabuni.
Anasema kila shule mpya 1 ilijengwa kwa Tsh,583,500,000.00 ambapo madarasa 112 mapya yamejengwa kwa Tsh,2,208,629,852.29 na mabweni likiwemo bweni la watoto wenye mahitaji maaluum lilijengwa kwa Tsh,1 28,000,000.00 na kupelekea madarasa kuongezeka kutoka asilimia 183 hadi 250.
Anasema mbali na fedha hizo toka serikali kuu kutumika kujenga shule za msingi,pia halmashauri kutumia mapato yake ya ndani waliweza kuongeza madarasa na kujenga matundu ya vyoo na baadhi ya shule mpya zimepewa majina ya viongozi wa wilaya.
Kavishe anasema mbali na ujenzi wa shule mpya na maboresho ya shule za msingi chakavu pia walipokea Tsh,5,883,760,056.00 toka serikali kuu zilizotumika kujenga shule mpya 4 zilizotumia Tsh,2,905,760,056 huku madarasa mapya 114 yakijengwa kwa Tsh,2,850,000.000,00.
Anasema ujenzi wa miradi hiyo umepelekea ongezeko la madarasa kutoka asilimia 129 hadi 243 mwaka 2025 na kuwa hiyo ni takwimu ya miaka 4 iliyopita chini ya utawala wa Rais Dkt,Samia Suluhu hali iliyoinua ufauru na kupunguza utoro,huku Kiasi cha Tsh,8,803,889,908.29 zikitumika kwa elimu msingi na sekondari.
Kavishe anasema mafanikio hayo yametokana na ushirikiano uliotukika kati ya Mbunge,mkuu wa wilaya,wakuu wa Idara na madiwani kuwa wasikivu huku wakipata sapoti kubwa kutoka kwa wananchi ambao awali watoto wao walitumia kilometa nyingi kwenda shule.
Anasema kwa sasa kila karibu kila kijiji kina shule ya msingi na kila kata inashule ya sekondari hivyo anataraji kuona wazazi wanawapeleka watoto shule kwa wingi ifikapo mwezi januari mwaka huu kwani elimu ni msingi na ufunguo wa maisha kila motto anapaswa kupelekwa shule.
Anaongeza kuwa anajisikia fahari kufanya kazi na mwenyekiti wa halmas hauri Abraham Sambira kwani amekuwa ni msikivu na mchapa kazi hali iliyopelekea wananchi wa Songwe umpa heshima kubwa na kuandika jila lake kwenye ukumbi wa mikutano ya halmashauri ikiwemo moja ya shule kitwa Abraham Sambila.
Aliongeza kuwa kwa upande wa Mbunge Phillipo Mulugo (Papaa Mukulu Mutu ya Watu) akishiriki kwa kila jambo kwani akiwa Bungeni alikuwa akiomba mara kwa mara kuondolewa kwa changamoto za elimu katika jimbo la Songwe na hata wananchi kuipa jina la Phillipo Mulugo moja ya shule mpya.
Anasema ana kila sababu ya kumshukuru Rais wa awamu ya Sita Dkt,Samia Suluhu kwa kusikia kilio cha wananchi wa wilaya ya Songwe ambapo kwa sasa wanafurahia shule mpya na ukarabati wa majengo chakavu hali iliyoongeza hali ya watoto kupenda shule.
Annastazia Mwashilindi Mkazi wa Mkwajuni,anasema mika mitano ya nyuma watoto wao walipata shida kubwa ya kutembea umbali mrefu kwenda kwenye kata zilizokuwa na shule walilazimika kutoipanda shule na kuona kama ni adhabu,lakini kwa sasa kila kata ina shule hali ya watoto kuipenda shule imeongezeka.
Shabbani Zefania mkazi wa Mbala anasema kipindi cha awamu ya sita wanafunzi wengi ufauru wao umengezeka kutokana na mabadiriko makubwa ya maboresho ya shule na kuwa anaamini wilaya hiyo mwakani ufauru utaongezeka mara dufu.
Saraphina Haonga mkazi wa Saza anasema ana kila sababu ya kumpongeza Mbunge Mulugo,Mwenyekiti Sambira mkuu wa wilaya na mkurugenzi kwani ushirikiano wao ndiyo sababu jimbo la Songwe kupaa kielimu huku akitaka kuona wilaya hiyo inakuwa ya kwanza kimkoa na kuingia 10 bora kitaifa kwa ufauru.








Comments
Post a Comment