JINSI JESHI LA POLISI MBEYA LILIVYOJENGEWA UWEZO MASUALA YA HAKI ZA BINADAMU.
Na Ibrahim Yassin, Songwe.
MAAFISA Wakaguzi na Askari wa vyeo mbalimbali wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya wamekumbushwa umuhimu wa kusimamia haki kipindi cha uchaguzi mkuu ili kudumisha amani na utulivu wa nchi.
Tanzania ni moja ya nchi yenye amani na utulivu hivyo ambyo ni tunu ya Taifa ,elimu iliyotolewa imewawapa mwanga zaidi maafisa hao kuzidi kuilinda amani iliyopo kwa kuzingatia haki za binadamu.
Rai hiyo imetolewa leo Septemba 22/2025 na Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Amina Ally wakati wa mafunzo ya masuala ya haki za binadamu na wajibu wa Jeshi la Polisi katika uchagu zi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Kamishna wa Tume Amina amesema kuwa, Tume ya haki za binadamu na Utawala Bora imepewa jukumu la kuhakikisha kila mwananchi ana haki ya kupiga kura katika hali ya amani na utulivu hivyo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Tume ina uhakika haki hiyo itatekelezwa bila upendeleo wa uwepo wa matumizi ya nguvu kupita kiasi.
Naye, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) amesema kuwa mafunzo hayo yatajenga ufahamu mkubwa kwa Askari kuhusu masuala ya haki za binadamu hasa katika kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi na uchaguzi wenyewe.
Aliongeza kuwa, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lipo makini na litahakikisha linaimarisha ulinzi na usalama na kwa yeyote atakayekiuka sheria na taratibu atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.
Kwa upande wake Afisa Uchunguzi Mkuu wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ndugu Emmanuel Ndosi ameeleza kuwa Jeshi la Polisi linao wajibu wa kulinda haki na kuhakikisha haki inatekelezwa hasa kipindi hiki cha uchaguzi kwa kutimiza wajibu wao kwa ufanisi na weledi ili kupunguza malalamiko.
Tanzania ipo kwenye harakati ya kufanya uchaguzi mkuu mwezi Oktoba mwaka huu hivyo maafisa wa haki za binadamu wanaendelea kutoa semina kwa waandishi wa habari na jeshi la polisi namna ya kutekeleza majukumu yao kwa kufuata misingi ya haki.






Comments
Post a Comment