POLISI ,TRA SONGWE WANASA PEMBE ZA NDOVU ZA ZAIDI YA MIL,240 KATIKA OPERESHENI ZAO.




Na Ibrahim Yassin, Songwe

Katika muendelezo wa Operesheni ya pamoja kati ya maafisa wa mamlaka ya mapato Tanzania na Jeshi la polisi mkoani Songwe walifanikiwa kuwa nasa watu kadhaa wakiwa na pembe za ndovu za zaidi ya milioni 240.

Operesheni hiyo kamata magendo ilifanyika kwa ushirikiano mkubwa baad a ya mamlaka ya mapato na jeshi la polisi kuendesha msako wa mara kwa mara katika mip aka ya Ileje na Malawi na ule wa Tunduma na Zambia.



Katika Doria hizo zilizofanyika siku za hivi karibuni kupitia nyia za vipenyo (za Panya zaidi ya 300) maeneo ya Tunduma Momba na Ileje kupitia mwa mbao wa mto Songwe bidhaa nyingi zilikamatwa yakiwemo meno ya tembo.

Kwa mujibu wa meneja msaidizi wa TRA mkoa wa Songwe Nsajigwa Mwa mbegele ni kuwa lengo la kuendesha Operesheni hizo ni kuhakikisha njia zote za Panya zinadhibitiwa itumike njia kuu pekee.

Amesema itakapo tumika njia kuu kupitishia bidhaa watalipisha maputo ya serikali kwa ufasaha na bidhaa zisizotakiwa kama pembe za ndovu na zinginezo zitakamatwa na sheria itaendelea kusimamiwa.



Amesema wamekuwa wakitoa elimu mara kwa mara kuhusu madhara ya kupitisha bidhaa halamu na na bado wanaendelea kutoa elimu hasa kwa wafanyabiashara kupitia jumuiya zao umuhimu wa kulipa kodi kwa hiyari.d

"TRA imepewa jukumu la kukusanya mapato ya serikali, ili tukusanye vizuri tunatakiwa tudhibiti uvushaji holela wa bidhaa kutoka nchi za Malawi na Zambia hasa pombe za viroba na vipodozi."amesema Mwambegele.

Nae Kamanda wa Polish mkoani Songwe Augostino Senga amesema jeshi la polisi halita lala, doria zitaendelea kufanyika usiku na mchana kuwa kamata wanaovunja sheria kwa kuingiza bidhaa haramu nchini.

Amesema serikali imewaongezea nguvu kwa kuwapatia magari 6 mapya yatakayotumika katika operesheni mbalimbali hivyo aliwataka watu wenye tabia ya kuvunja utaratibu uliowekwa na serikali ikiwemo kusafirisha pembe za ndovu waache mara moja.




"Tufuate sharia zilizopo, serikali imekataza kuingiza bidhaa haramu zikiwemo pombe za viroba, pia usafirishaji wa pembe za ndovu umepigwa marufuku,ni bora wenye biashara hizo wabadirishe maana watakamatwa na kupelekwa kwenye vyombo vya sheria "amesema.

Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa