JAMII YATAKIWA KUTOJICHUKULIA SHERIA MKONONI
Na Ibrahim Yassin, Songwe.
JAMII Nchini imetakiwa kutojichukulia sheria mkononi na badala yake imetakiwa kufuata sheria zilizowekwa ili kuhepuka mauaji yasiyo ya lazima.
Kauli hiyo imetolewa jana na mkuu wa polisi jamii mkoa wa Songwe Maria Kway wakati akizungumza na Wananchi wa Kitongoji cha Kamficheni, Kata ya Magamba, Wilaya ya Mbozi Mkoani hapa
Kamishna Msaidizi (ACP) Kway, alitoa elimu kwa wananc hi hao kuhusu mas uala ya ulinzi shiri kishi, maadili, na ushirikiano wa kijamii kama njia ya kuimarisha usala ma wa maeneo yao.
Katika Elimu hiyo, ACP Kway aliwaku mbusha wananchi juu ya madhara ya kuozesha wanafu nzi na kuwataka kulinda haki za watoto ikiwa ni pamoja na kuach ana na mila na imani potofu zinaz okiuka haki za binadamu, huku akiwataka wazazi kuwajibika ipasavyo katika malezi na makuzi ya watoto kwa manufaa ya maisha yao ya baadae.
Aidha, ACP Kway alikemea vitendo vya ubakaji na ulawiti na kuwata ka wazazi kutoku walaza watoto na wageni au ndugu wanaowatembele ili kuepusha watoto kutokufanyiwa vitendo vya kikatili.
Aidha amewasisitiza wananchi hao kujishughulisha katika shughuli halali za kujipatia kipato na kuendesh a maisha yao ya kila siku kwa kufiata misingi ya kitanzania.
Aidha, ACP Kway aliwataka wananchi hao kusalimisha silaha zinazomili kiwa kinyume cha sheria kwa kipindi hiki cha msamaha wa usalimishaji wa silaha, huku akiwao mba kuendelea kudumisha amani wakati, na baada ya uchaguzi ikiwa ni pamoja na kushi rikiana kutatua changamoto za kijamii kwa njia ya amani na kufuata utaratibu wa kisheri a.
Katika kuhitimisha elimu aliyokuwa anaitoa, ACP Kway alisisitiza kuwa hali ya usalama ni jukumu la kila mmoja, na hakuna maendeleo bila amani na mshikam ano huku akiahidi kuwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe litaendelea kushiri kiana na wananchi katika kuhakikisha jamii inakuwa sala ma, yenye nidhamu na na kuzingatia sheria.
Mwisho.



Comments
Post a Comment