Halmashauri Nkasi yapokea boti kwa ajili ya huduma za chanjo
Na Israel Mwaisaka, Rukwa
Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi imepokea boti kutoka Wizara ya Afya ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuboresha utoaji wa huduma za afya hususani utoaji chanjo katika maeneo yaliyopo mwambao mwa Ziwa Tanganyika.
Kupatikana kwa boti hiyo kutarahisisha utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Afya ikiwemo usambazaji wa chanjo, usimamizi wa huduma za chanjo pamoja na utoaji wa huduma mkoba katika vituo vya kutolea huduma za Afya vilivyopo mwambao mwa ziwa Tanganyika.
Msaada huu ni hatua muhimu katika kuhakikisha watoto na wananchi kwa ujumla wanaoishi katika maeneo ya mwambao mwa ziwa Tanganyika wanapata huduma bora za kinga dhidi ya magonjwa yanayozuilika kwa chanjo, sambamba na kuboresha usimamizi wa huduma hizo kwa ujumla.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya Nkasi Afraha Hassan kwa upande wake amemshukuru Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk,Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyoendelea kuhakikisha upatikanaji wa huduma Bora za afya kwa Wananchi wa wilaya Nkasi
Alisema kuwa kulingana na mazingira ya ukanda wa ziwa Tanganyika jiografia ya maeneo hayo Ni ngumu na ku
pelekea Wagonjwa kushindwa kupata huduma za afya za uhakika hasa zile za dharura na huduma za chanjo hivyo boti Kama hiyo huwa Ni suluhisho kubwa la changamoto hizo.
Licha ya boti hiyo iliyotolewa na serikali kujikita zaidi katika eneo la chanjo pia itatumika Kama "ambulance" pale anapopatikana magonjwa wa dharura anapohitaji huduma za juu katika vituo vya afya na kuendelea

Comments
Post a Comment