GEORGE MSYANI AZINDUA KAMPENI WANANCHI WAITIKA WAKIWA NA OMBI LA MAJI
Na Ibrahim Yassin ,Vwawa
MGOMBEA udiwani kata ya Nanyala Jimbo la Vwawa wilayani Mbozi Mkoani Songwe George Msyani leo Amezindua kampeni tayari kwa kuaomba kura za ndiyo kwa wananchi.
Msyani ambaye awamu iliyopita alikuwa diwani na mwenyekiti wa halmashauri wilayani Mbozi amezindua kampeni akitete nafasi yake kwa awamu nyingine.
Katika uzinduzi huo uliohudhuriwa na viongozi wa ccm ngazi za vitongoji.vijiji na kata wkiwemo waliogombea udiwani ambao kura zao hazikutosha walifika kumuunga mkono.
Katibu wa ccm kata ya Nanyala Abel Zizya alitambulisha wageni huku katibu wa siasa itikadi na mafunzo wa kata Kilian Nwashilindi akisherehesha na kuufanya uzinduzi huo wa kampeni kunoga zaidi.
Mwenyekiti wa kata hiyo Tangili Mwashalawe aliuelkeza umma huo kuwa kata ya Nanyala imenoga miradi mingi imejengwa changamoto zilizo salia anaamini zitatuliwa awamu ijayo.
Pendo Mwaitwalile mkazi wa senjele amesema anakila sababu ya kumpongeza mgombea huyo kwani awamu iliyopita miradi mingi ikiwemo ya elimu na afya imejengwa huku akiwa na ombi la kutatuliwa changamoto ya maji eneo hilo.
Asajile Kayange mwenyekiti kijiji cha Senjele amesema bado anaimani na George Msyani kuendekea kuiboresha kata hiyo.
Mgombea udiwani viti maalum tarafa ya Iyula Mesia Swela amesema
Katika Kata hiyo kulikuwa na wagombea 7 walioingia kuomba kura za maoni ambapo wajumbe walimpitisha George Msyani anaye peperusha bendera ya chama akiwa mgombea pekee .
George Msyani mgombea udiwani amesema walikuwa 7 sasa amepita yeye hivyo ushindi huo ni wa chama.
Amesema kata hiyo ni mpya ilimegwa toka kata mama ya Luanda ikiwa na changamoto nyingi.
Amesema awamu iliyopia amejenga amefanikisha mengi ikiwemo shule na zahanati kero iliyopo ni maji.
Amesema wakati anaingia hakukuwa na maji lakini kwa sasa maji yapo asilimia 40 awamu ijayo akipata ridhaa atahakikisha upatikanaji wa maji unakuwa asilimia 100.
Mabadiliko tabia nchi na matumizi ya uharibifu wa mazingira sababu vyanzo vya maji kuwa vigumu lakini mikakati imepangwa kuhakikisha tatizo la maji linamalizika.


Comments
Post a Comment