DARASA LA COMPUTER SECONDARI YA SUMAGHA KULETA TIJA YA KUJIAJILI,SOMO LAINGIZWA KWENYE MTAALA.
"Wazazi, walezi,leteni wanafunzi wapate masomo ya (pree form One) nipigieni 0745437195 shule ya SUMAGHA inafaurisha darasa zima,tumefanikiwa kuitokomeza alama 4 na sasa tutaitokomeza alama 3 tubaki na One na Two." Kapela ,mkuu wa shule.
Na Ibrahim Yassin, Songwe,
Wazazi na walezi nchini wametakiwa kuwapeleka wananafunzi kujiunga na kidato cha kwanza kwa msimu wa mwaka 2025/26 ili wapate elimu bora na sahihi kwani shule hiyo inadarasa la Kompyuta inayowao ngezea tija wanafunzi.
Imekuwa ni kawaida kwa wanafunzi wanapokosa nafasi ya kujiunga kidato cha 5 kushidwa kujiajiri lakini shule hiyo imeweka somo hilo kwenye mtaala kuwezesha wanaopenda somo hilo waweze kuendelea nalo hadi chuo.
Akizungumza Leo na Dira kamilifu mwalimu wa darasa la Kompyuta Cleanuell Amani amesema shule hiyo imeamua kuweka darasa la Kompyuta na kuliingiza kwenye mtaala ili kuwa wezesha wanafunzi kusoma Technology na wale watakaotaka kuendelea nalo wafike hadi vyuo vikuu.
Amesema pindi wanapohitimu kidato cha 4 wanapewa vyeti kama masomo mengine na kizuri zaidi wanafunzi wanaelewa na wanapenda kusoma, kipindi hiki cha maandalizi ya kidato cha kwanza wameongeza ufanisi zaidi wa somo hilo.
Mariam Mtafya mkazi wa Ileje amesema anajisikia fahari mwanae wa kidato cha 3 anapokuja likizo nyumbani anaitumia vizuri Kompyuta huku akiongea Lugha za kigeni zaidi ya 3 na kuwa anauhakika mitihani ya kuhitimu kidato cha 4 atapata division one.
Mkuu wa shule hiyo Mwl,Evodius Kapela amesema wameamua kuweka darasa la Kompyuta ili wanafunzi wanapotoka hapo waweze kupata ajira na kujiajiri na pia hata wakiendelea na kidato cha tano hadi vyuo watakuwa na uelewa mzuri.
Amesema shule hiyo kwa Miaka 6 mfululizo imekuwa inafaulisha wanafunzi wote na kwamba hakuna alama 4 wala 0 na kuwa mkakati uliopo ni kutokomeza alama 3 wabaki na alama One na Two,na bado wanapokea wanafunzi wa kuhamia.




Comments
Post a Comment