ASKARI POLISI ALIYEUMIA AKIWA KAZINI AKABIDHIWA BAJAJI.



Na Ibrahim Yassin, Songwe 

KAMANDA wa polisi mkoa wa Songwe,  Augostino Senga amemkabidhi bajaji Konstebo Haruna ili imsaidie katika shughuri zake za kila siku baada ya kupata ulemavu akiwa kazini. 

Kamanda Senga amekabidhi bajaji hiyo jana akimuwakilisha mkuu wa jeshi la polisi nchini  (IGP) Camilius Wambura ili bajaji hiyo imsaidie afande Haruna katika majukumu yake. 

Makabidhiano ya bajaji hiyo yalifanyika nyumbani kwa askari huyo Septemb a 19/2025 huku ikishuhudiwa na askari kadhaa. 

Baada ya kukabidhi zawadi hiyo Kamanda Senga amesema hatua hiyo ni udhibitisho kuwa jeshi la polisi linatambua na kuthamini  mchango wa askari wake.

Na pia Kamanda Senga alimueleza afande huyo kuwa hasikate tamaa kwani uongozi wa Jeshi hilo upo tayari kumjali na kumsaidia pale atakapo kuwa na changamoto zozote.



Kwa upande wake Constebo Haruna alitoa shukrani kwa uongozi wa jeshi hilo chini ya IGP Wambura kwa kuwa na upendo uliotukuka na kusema bajaji hiyo itamsaidia kwenye mizunguko yake. ya kwenda kazini hasa kuendeleza shughuri zake. 

"Bajaji hii itanisaidia kwenda kazini na kurudi nyumbani na kuendesha shughuri zangu kwa ufanisi zaidi licha ya ulemavu nilionao, naupongeza uongozi wa jeshi kuona umuhimu wa kunisaidia "amesema afande Haruna.

Hata hivyo tukio hilo limeonesha wazi jinsi jeshi la polisi linavyo wajali wafanyakazi wake na hata baada ya wao kuathirika katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku kulinda usalama wa raia na mali zao.




Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa