Makada 26 wa CCM wilaya Nkasi waliochukua fomu za kuwania Ubunge wamefanikiwa kuzirejesha
Na Israel Mwaisaka,Nkasi
Makada 26 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Nkasi waliochukua fomu za kuwania Ubunge Katika majimbo yote ya wilaya Nkasi wamefanikiwa kurejesha fomu.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jana ofisini kwake katibu wa CCM wilaya Nkasi Anastazia Almasi amesema kuwa Toka mchakato wa uchukuaji fomu uanze June 28,2025 na kumalizika Leo Julai 2,2025 Wanachama wa CCM wapatao 26 waliochukua na fomu na kuwa wote waliochukua wamefanikiwa kuzirejesha fomu hizo.
Amesema kuwa wilaya Nkasi inaundwa na majimbo mawili ya uchaguzi ambayo ni Nkasi kusini na Nkasi Kaskazini ambapo Katika Jimbo la Nkasi kusini waliochukua fomu walikuwa 12 na Nkasi Kaskazini 14 na kuwa hadi zoezi Hilo linapofungwa Leo Julai 2,2025 makada wote walizochukua fomu hizo wamefanikiwa kuzirejesha.
Amewataja makada hao waliochukua na kuzirejesha fomu katika Jimbo la Nkasi kusini kuwa ni Moses Kaegele, Desderius Mipata, Godfrey Stima Kalembe, Christopher Evarist Mwanansao,Selis Ndasi,Joseph Evod Walingozi, Audats Salvatory Kisato,Paul Vincent Mbogo,Revania Credo Misonje,Lameck Kostantino Nkana,John Joseph Chota na Alphonce Albert Stima.
Kwa upande wa jimbo la Nkasi kaskazini ni David Ndilo Siame,Bazilio Kapunda Mbwilo,Keissy Salum Sood Aljabri,John Joseph Sichilima,Jastus Ernest Shauri,Pascal Francis Mwakatenya,Thomas Leopod Kalunga, Boniface MwanduLugwisha,Jonas Leando Kifunda,Saadan Seif Nassoro Shibiby,Ally Mohammed Kessy,Lameck Peter Kafungawazi ,Salumu Kazukamwe na Isaya Robert Kapela.
Katibu huyo wa CCM amefafanua kuwa baada ya zoezi Hilo la uchukuaji na urejeshaji wa fomu kukamilika Leo ni kuwa sasa michakato mingine itaendelea ya uchujaji wa majina kupitia vikao mbalimbali vya chama kwa mujibu wa katiba na kanuni zilizowekwa na chama hicho.
Amedai kuwa kwa mujibu wa ratiba Julai 4 kamati za siasa za kata zitakaa kujadili waombaji wa nafasi za Udiwani,Tarehe 5 Kamati ya utekekezaji ya wilaya itajadili majina ya Udiwani wa viti maalumu na Tarehe 6 Kamati ya siasa ya wilaya itajadili majina ya Udiwani ngazi ya kata, Madiwani viti maalumu na Wagombea Ubunge ngazi ya jimbo.
Amesema kuwa baada ya vikao mbalimbali vya kisheria ngazi ya wilaya kukamilisha mchakato wa uchujaji wa majina katika ngazi zote za Udiwani na Ubunge watayapeleka majina hayo mkoani ambapo vikao vya mkoa vitaanza kuketi Tarehe 8 ya mwezi huu.







Comments
Post a Comment