WANANCHI ILEJE WACHEKELEA OFISI YA BIL,3.834 WALIYOIKOSA TOKA MWAKA 1975.



Na Ibrahim Yassin,Ileje

WANANCHI wilayani Ileje mkoani Songwe,wamepongeza serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt,Samia Suluhu kwa kujenga ofisi ya kisasa ya halmashauri itakayoongeza hamasa ya utumishi wa umma.

Halmashauri hiyo ilianzishwa mwaka 1975 ikiwa haina ofisi huku ikitumia majengo ya mkuu wa wilaya ambapo mwaka 2019 ilihamia kwenye ofisi zake kutokana na idadi ya watumishi kuwa kubwa.





Akizungumza leo wakati wa ziara ya katibu tawala wa mkoa,mkurugenzi wa halmashauri hiyo Nuru Kindamba amesema walipokea Tshs,3,834,1 48,401.50 toka serikali kuu kujenga ofisi ya kisasa ya halmashauri hiyo itakayokuwa na huduma za idara zote.

Amesema kati ya fedha hizo Bill,2 zimetumika katika ujenzi wa awamu mbili ambapo kila awamu ilitumia Bilioni 1 ambapo mkandarasi anayejenga akiwa ni Mbuya Contrators.



amesema mradi utakapo kamilika utaongeza ufanisi wa utoaji wa huduma kwa wananchi na kuboresha mazingira ya kazi kwa wananchi ambapo kwa sasa upo hatua ya umwagaji wa zege la nguzo wima..

Katibu tawala mkoani Songwe Happiness Seneda alipongeza hatua ya ujenzi huku akimtaka mkandarasi azidi kuongeza kasi ili mradi ukamilike kwa muda uliopangwa.

Hata hivyo mradi huo utakapokamilika utaiweka wilaya ya Ileje katika mazingira mazuri kutokana na awali kutumia majengo chakavu kama ofisi huku wakimpongeza Rais Dtk, Samia Suluhu kwa kuwapatia fedha hizo.

Seneda alienda wilayani Ileje akitopkea Mji wa Tunduma katika ziara yake ya kikazi ambapo kesho atakuwa wilaya ya Mbozi kwa ajili ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.




Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa