VIJANA/WANAWAKE WANATAKIWA KUINGIA KWENYE KILIMO CHA KAHAWA KUJIKWAMUA KATIKA LINDI LA UMASIKINI.

                       MAKALA
.Wengi  wanadhani kilimo cha Kahawa ni cha Wazee

N a Ibrahim Yassin,Songwe

WITO umetolewa kwa vijana na wanawake kujiingiza kwenye kilimo cha zao la Kahawa ili kujiingizia kipato badala ya kuwaachia wazee pekee hali itakayosababisha kilimo hicho kudhorota pindi wazee watakapofariki.

Imekuwa ni kawaida kwa wanajamii wengi kudhani kulimo cha Kahawa ni cha wazee pekee huku vijana na wanawake wengi wakillima mazao mengine ya muda mfupi hali inayotakiwa hamasa zaidi itolewe ili vijana hao waanze kulima kahawa.

Zao la Kahawa ni moja ya mazao yenye uchumi  mkubwa nchini na dunia kwa ujumla hali inayotakiwa vijana kuingizwa kwenye kilimo hicho ili wajifunze jinsi wazee wao wanavyolima na hata wazee watakapotoweka duniani kilimo kiendelee.



Kauli hiyo imetolewa na Ezekiel Mwakyoma meneja wa kanda ya mbeya wa bodi ya Kahawa (TCB) wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake akielezea mpango mkakati waliojiwekea kuhakikisha zao la Kahawa linalimwa na watu wa lika zote.

Anasema Bodi ya Kahawa imeundwa kwa sheria namba 23 ya mwaka 2001 na kufanyiwa marekebisho ya sheria za mazao namba 20 ya mwaka 2009 inayowapa mamlaka ya kusimamia sekta ya Kahawa kwa kufuata kanuni na sheria ya kuratibu shughuri zote.

Kutokana na hali hiyo wamejipanga kuhakikisha zao la Kahawa linaongezeka kwa kuongeza hamasa kwa vijana na wanawake kuingia zaidi kwenye zao hilo ili hata wazee wao watakapo toweka ama kustaafu  vijana wawe wamepata uzoefu wa kuliendeleza zao hilo.

‘’Kazi kubwa tuliyonayo ni kuhakikisha tunatoa hamasa kwa wasiolima Kahawa walime,kuhamasisha taasisi tunazofanya nazo kazi zinapanda miche zaidi ili wakulima wasikose miche lengo ni kuongeza tija ili pato la wakulima na serikali lipae mara dufu’’anasema.

Anasema wakati ongezeko la kahawa linakuja pia wapo kwenye mikakati ya kuweka mazingira bora kwa wakulima wa Kahawa na masoko ikiwemo zoezi la usindikaji na kulinda ubora wa Kahawa na kuwa kinara Afrika  ili iweze kuwa na ushindani mkubwa kwenye soko la Dunia.

Anasema ili Kahawa iendelee kuwa bora na mkulima asipate hasara wanahamasisha wakulima kupanda mbegu chotara aina ya Compact,inayoimili magonjwa ya Coffee Barry Disease(CDB) na Coffee Leat Rust (CLR) ukilinganisha na ile ya zamani (Local variety).





Anasema Mbegu ya Compact chotara inauwezo wa kustahimili ukame na inazaa kuanzia mwaka mmoja hadi mmoja na nusu huku ikitoa mazao mengi ukilinganisha na mbegu zingine ndiyo maana wanahamasisha wakulima kupanda

Anasema  Kahawa uzalishaji wake ulishuka kutokana na mabadiliko ya Tabia ya Nchi,ndiyo maana wameanza kuhamasisha uchimbaji wa visima ili pindi mvua inapokata mapema maji hayo ya visima yaanze kutumika kumwagiliwa mashambani.

Sambamba na hilo,Mwakyoma pia anasema wamekuwa wakitoa elimu na kusisitiza wakulima wapande mazao mseto (Mazao mchanganyiko ) ambayo ni Mcadonia,Parachichi,Migomba,Kahawa na miti ya kivuli ambayo ni rafiki ili waongeze kipato kwa kuvuna mazao ya kila aina.

Anasema ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na afya ya udongo,halmashauri zote kupitia maafisa ugani wamekuwa wakipita kwa wakulima,wakipima afya ya udongo na kutoa ushauri kutumia mbegu za asili ili kulinda afya ya udongo.

Ansema lengo la elimu hiyo ni kufanikisha lengo la kila mche mmoja utoe kilo 2 badala ya gramm 200 ambayo ni nje ya lengo na kwamba mwaka 2024/25 walikusanya Tani, 20,870.6 kahawa ghafi nje ya matarajio ya tani 30.000 na kuwa tayari wameweka malengo ya kupata tani 50.000.
‘’Ili kufanikisha hilo,wanashirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo taasisi ya utafiti wa mbegu (TAcRI) Kanda ya Mbeya,pamoja na halmashauri kupitia idara za kilimo ambao ndiyo wanaowajua wakulima katika maeneo yao’’Anasema.

Afisa ubora kutoka bodi ya Kahawa kanda ya Mbeya Frolian Ndungulu anasema waliweka mahitaji kuanzia mwaka 2020 hadi 2025 kahawa ipate soko la uhakika kutokana na kuongeza thamani ya ubora ambapo awali ulikuwa chini.



Anasema wanaendelea kutoa elimu kwa wakulima kuzingatia kanuni 10 za ubora na tayari wameanza kuzingatia huku lengo lao ni kuwa na asilimia 70 ya ubora ukilinganisha na uliopo sasa wa asilimia 35 na kuwa kwa upande wa vijana ni asilimia 25 tu ndiyo wanaoshiliki kilimo.

Kajilu Francis mkurugenzi wa maendeleo ya mazao na uendeshaji nchini anasema wamejipanga kuhakikisha kahawa nchini inakuwa na ushindani zaidi katika soko la Dunia na kwa kufanikisha hilo,wameanza kuchimba visima vya maji mashambani ili mvua zikikata maji hayo yatumike kwenye umwagiliaji wa Kahawa.

Anasema tayari kwa wilaya ya Mbozi visima 10 vimechimbwa na kufungwa mota na kuwekwa minara ya sola kati ya hivyo visima vinne havukuwa na maji ambapo wamevirudia tena kuvichimba,hadi sasa visima viwili vimekamilika na viwili vipo hatua za mwisho.

Anasema mwaka 2021 hadi 2025 waliweka malengo ya kukusanya Kahawa tani 300.000 na kuongeza ubora asilimia 75 na kuwa kila eneo la uzalishaji kahawa ina ubora wake na kukubarika sokoni kutokana na uhitaji wa wateja wanaohitaji aina gani ya kahawa.

Anasema Kilimo kinachangia asilimia 24 ya pato la Taifa lengo walilojiweke a ni asilimia 30 na tayari wamejipanga kuiongeza uzalishaji,kutoa mafun zo,kuchimba visima kuongeza tija kwa kupanda mbegu chotara za Compact.

Ifahamike kuwa ili kahawa izidi kupaa ipo haja wakulima kuondolewa changamoto zinazowakumba ikiwemo kuwawaishia pembejeo zikiwemo mbolea ili wafanya maandalizi zaidi mashambani.


Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa