MSANII WA BONGO FLEVA AWAASA WASANII KUTUNGA NYIMBO ZA KUELIMISHA JAMII,KUPINGA UNYANYASAJI WA KIJINSIA NA RUSHWA YA NGONO.



‘’Imekuwa ni kawaida kwa wasanii wengi kumba nyimbo za mapenzi badala ya kuimba za kuelimisha jamii kupinga ukatili na unyanyasaji wa kijinsia,ikiwemo rushwa ya ngono.’’

Na Ibrahim Yassin,Songwe

MSANII wa Bongo Fleva ,Deo Samson Mnkondya (TS MONEY) amewataka wasanii nchini kutunga na kuimba nyimbo za kuelimisha jamii na kupinga ukatili na unyanyasaji wa kijinsia na rushwa ya ngono badala ya kuimba nymbo za mapenzi pekee.

Mnkodnya ameyasema hayo jana wakati wa mahojiano na waandishi wa habari ofisini kwake huku akijiandaa kuachia nyimbo mbili zinazopinga ukatili wa kijinsia.



Alisema baadhi ya jamii nchini wamekuwa wakikumbwa na matatizo mengi yakiwemo ya unyanya saji wa kijinsia na hata wa kingono,hivyo kuna kila sababu ya wasanii kupinga mambo hayo kwa kutumia musiki badala ya kuiachia serikali pekee.

Mnkodya anayetamba na kibao kikali cha ‘’Kitoto ‘’inayoimbwa katika vituo mbalimbali vya redio nchini,alisema ametunga nyimbo mbili za kupinga ukatili ambazo zipo katika hatua za mwisho kuachiwa huku akitarajia ujumbe uliomo kwenye nyimbo hizo utapunguza ama kumaliza kabisa mambo ya ukatili ya kijinsia.

Alisema licha ya nyimbo nne alizoachia kutikisa kwenye vituo mbalimbali vya redio,ambazo ni Kitoto,Habibi,Kibubu ,Neema na Nitazoea, pia yupo mwishoni kuachia nyimbo 2 zinzzoeleza kuhusu ukatili wa kijinsia wanaofanyiwa baadhi ya wanawake hapa nchini.

Msaanii huyo aliyezaliwa Aprili 10/1992 katika mji wa Vwawa alisema alianza kuimba mwak 2009 akiwa msanii wa kujitegemea na alifanikiwa kuimba nyimbo ya NEEMA uliofanya vizuri na kupokelewa vizuri mitaani hadi sasa bado unasikika.



Alisema hadi sasa nyimbo zake nyingi zinapatikana katika Platform za miziki na kwenye vituo mbalimbali vya redio na televisheni na kwamba anawomba washabiki waendelee kumpa sapoti na kusikiliza nyimbo zake zilizopo kwenye istagram na mitandao mingine wakianza na neno TS money.

Alimaliza kwa kusema kuwa mbali na nyimbo zake kuwa kwenye mitandao ya kijamii, mashabiki wajiandae kusikiliza nyimbo zake mpya zilizoimbwa kwa utetezi na kupinga unyanyasaji wa kijinsia na rushwa ya ngono kwa watoto wa kike.






Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa