MIKIKI MIKIKI YA KISIASA JIMBO LA VWAWA NA MBOZI,WADAU WALITAJA JINA LA MDALAVUMA NGULI WA SIASA NCHINI.
‘’Mdalavuma anawajali watu,miaka 10 iliyopita watu wake walitembea kilometa 56 kusaka tiba wengi wao walitibiwa kwa waganga wa jadi,lakini amejenga zahanati 4 na kituo cha afya,tupo kumsahwishi agombee ubunge’’
Na Ibrahim Yassin,Songwe.
Katika kuelekea uchaguzi mkuu mwezi Octoba mwaka huu,wadau wa siasa wilayani Mbozi mkoani Songwe wamemuomba Diwani wa kata ya Bara tarafa ya Itaka wilayani hapa Chief Aloyce Mdalavuma kujiandaa kuchukua fomu ya kugombea moja ya majimbo wilayani hapa.
Wilaya ya Mbozi yenye majimbo mawili yaani jimbo la Vwawa na Mbozi baadhi ya wadau katika majimbo hayo kwa nyakati tofauti,wamemuomba mwanasiasa huyo kuchukua fomu ya kugombea ubunge moja ya jimbo wilayani humo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wilayani humo wadau hao wamesema nguli Aloyce Mdalavuma anasifa zote za kuwa Mbunge kwani wameona jinsi alivyoitumikia kata ya Bara alikoshiiiriki shughuli za maendeleo katika kila idara.
Asifiwe Mwampashi mkazi wa Vwawa alisema alitembelea katika jimbo hilo na kujionea jinsi alivyojenga Zahanati katika vijiji vyote zikiwemo shule 4 za msingi na moja ya sekondari ikiwemo High Shool na kituo cha afya ambavyo ujenzi wake upo hatua za mwisho.
Nae Anne Kayange mkazi wa Mbozi alisema Chief Mdalavuna anasifa zote ikiwemo utashi wa kisisa,utu,ukarimu,ushawishi na hata kuwajali wananchi ambapo katika kata ya bara miaka 10 iliyopita wananchi wakiwemo mama wajawazito walitembea umbali wa kilometa 56 kusaka tiba.
Alisema afya ndiyo kila kitu katika maisha ya watu,kwa kuliona hilo alijenga zahanati kila kijiji,na kujenga kituo cha afya kunusuru watu wake kutembea kilometa 56 hadi wilayani kutibiwa ambapo watu wengi walitibiwa kwa waganga wa tiba za jadi.
‘’Tuna kila sababu ya kumsawishi Mdalavuma agombee ubunge kati ya jimbo la Mbozi au Vwawa ili alichokifanya kata ya Bara.akifanye kwenye moja ya jimbo atakalogombea kwani tayari wamejenga imani nae’’alisema Kayange.
Salama Mwashilindi mkazi wa Bara alisema yeye wakati Mdalavuma anagomea udiwani hakumpa kura yake,lakini jinsi alivyoibadirisha kata hiyo anajuta kwanini alimnyima kura,kitendo cha wadau kuomba agombee ubunge kinamashiko.
Alisema mbali na kuiletea maendeleo kata ya bara,pia amezifungua barabara zote zilizokuwa na changamoto na kuzilima mpya,huku akiwaasa wananchi wake wajiingize kwenye kilimo cha Kahawa ili wawe na uchumi wa uhakika.
;;Ndugu mwanahabari,Chief Mdalavuma ni mwanasiasa nguli nchini na ni mmoja wa madiwani makini kuwahi kutokea katika historia ya madiwani bora nchini,nilimfuata nyumbani kwake kumueleza jinsi wadau wanavyotaka agombee ubunge lakini hakuweza kusema chochote zaidi ya kusema anashukuru kwa ushauri’’alisema.
Kwa upande wake Chief Mdalavuma alipotakiwa kuzungumzia mapokea ya maombi ya wadau hao,alisema ni kweli amefuatwa na makundi mbalibali lakini hajaweza kuwajibu chochote kwa kuwa muda bado na pia hajafikilia kugombea ubunge.
Alisema hawezi kusema chochote kwani kanuni za chama cha mapinduzi haziruhusu kuzungumzia ubunge wakati majimbo yote yana wabunge tena watokanao na chama chake hivyo muda ukifika atawajibu wadau hao kuwa atagombea au laa.



Comments
Post a Comment