Jamii imetakiwa kuwa na utamaduni wa kusoma dua na kumshirikisha Mungu kwa kila jambo
- Get link
- X
- Other Apps
Na Ibrahim Yassin,Songwe
JAMII nchini imetakiwa kuweka utamaduni wa kusoma Dua kumuomba mungu ikiwemo kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia,rushwa,mauaji ya arbino na vitendo vingine visivyofaa ili Mungu aweze kutoa Baraka zake na kuifanya nchi kuendelea kuwa salama.
Batuza alisema kuna kila sababu ya kudumisha na kuilinda amani iliyopo kwa kumuomba mungu na kumshirikisha katika kila jambo kwani zipo nchi kadhaa duniani zinatamani amani iliyopo nchini hivyo kuna kila sababu ya kuongeza kuomba dua kwa Mungu ili amani iendelee kuwepo.
Mjumbe wa Halmashauri kuu wa baraza kuu la waislam (BAKWATA) mkoani Songwe,Abdallah Bakari alisema wameona kuna umuhimu wa kufanya dua ili kuihepusha nchi na maadui wakiwemo baadhi ya wanasiasa na kwamba Mungu anawapenda wanaoomba Dua na anawachukia wasio omba.
Anuar Ashraff Khan katibu wa baraza kuu la waislam ( BAKWATA ) mkoani Songwe,alisema wameamua kusoma dua ili nchi na viongozi wazidi kuwa salama na ni kawaida yao kufanya hivyo,na kuwa katika dua hiyo wamewashirikisha wachungaji,viongozi wa serikali na wazee wa mila.
Nae Sheikhe Nasoro Abdallah Msham Amili wa kanda ya nyanda za juu kusini,alisema waislam toka enzi ndiyo wenye utamaduni wa kuombeana amani wakitumia neno Asalam Aleykum (Amani iwe juu yenu),ma jibu Waleykum Salaam (Nanyi pia) na katika Surat Bakara yenye herufi 25,500 za maneno inazungumzia amani wakati Nabii Ibrahimu anaenda mji wa Makka akiisoma.
Alisema Wakati Nabii Mohammad alipoitwa na Mungu Mbinguni kupewa nguzo tano za sala alipofika mbingu ya saba alitokewa na Mungu akimpa salam ,,Asalaam Aleykum yaa Muhammad,Mtume akajibu Waleyku m Salaam Yan haa, hivyo na kuwa kuhusu amani waislam kwao ni Ibada hivyo izidishwe ili amani yetu iendelee kuwepo.
‘’Rais Dkt,Samia na watendaji wake wa serikali na taasisi zingine tunawaombea Dua ili Mwenyezi mungu awafanyie wepesi wawe na afya bora wapate ulinzi ili waendelee kulitumikia Taifa hili huku Mungu akiendelea kuwalinda.
Immam wa msikiti wa Istikama Bakari Tugenja alisema wameungana pamoja kusioma dua kuiombea nchi na viongozi wake,Mungu alisema katika Qur an tukufu ADIUN ASTAJIBU LAKUM,(Niombeni mimi nitakujibuni )
Askofu Gaison Mwanja wa kanisa la Agano la ukombozi lililopo Tunduma,alisema kuna umuhimu wa kufanya Dua,na kwamba wameungana na waislam kutii agizo la Mungu lengo ni kuihubiri amani na si udini.
Kiongozi wa wazee wa mila Chief Sibhelwa Nzunda alisema suala la kuiombea amani nchi ni la kila mtu,wao wameungana na waislam katika kusoma dua wakiwa na lengo la kutaka nchi na viongozi wake wendelee kuwa salama.
Alisema waka kama wazee wa mila na wajumbe wa kamati ya amani ya mkoa wa Songwe,wamekuwa kipaumbele kuomba dua,kupinga vitendo vya kiharifu,unyanyasaji wa kijinsia,utekaji na mauaji ya watu wenye Ualbino,na kuwa wataendelea kushirkiana na taasisi zote kuhakikisha amani inaendelea kudumishwa.
- Get link
- X
- Other Apps



Comments
Post a Comment