DC NKASI-ATAKA UBORESHAJI WA BWAWA LA MFILI KWENDA SAMBAMBA NA UHIFADHI WA PORI LA MFILI AMBACHO NI CHANZO KIKUU CHA MAJI
Na Israel Mwaisaka,Rukwa
Mkuu wa wilaya Nkasi Peter Lijualikali amesema kuwa jitihada zinazofanyika sasa za kuhifadhi Bwawa la Mfili kama chanzo kikuu cha maji katika mji wa Namanyere kiendane na kuutunza msitu wa Mfili ambacho ndicho chanzo kikuu cha maji katika Bwawa hilo.
Hayo ameyasema jana kwenye mkutano wa wadau kwa ajiri ya utambulisho wa Uhifadhi wa Bwawa la mfili ambapo ameitaka bodi ya bonde la ziwa Tanganyika kwamba inapofikilia kulitunza Bwawa la Mfili pia wawe na mkakati wa kuulinda msitu wa mfili ambacho ndicho kiwezeshi kikubwa cha maji katika Bwawa hilo.
Pia amewataka viongozi wa vijiji na vitongoji wanaouzunguka msitu huo wa Mfili kuwa mstari wa mbele katika kuielimisha jamii juu ya umuhimu wa msitu wa Mfili katika kusitawisha Bwawa la Mfili kama chanzo kukubwa cha maji katika mji wa Namanyere.
Alidai kuwa vuiongozi wa vijiji,vitongoji na kata moja kati ya jukumu lao la msingi ni kulinda hifadhi ya mazingira katika maeneo yao na kuhakikisha wale wote wanaovamia vyanzo vya maji wanadhibitiwa mapema badala ya kusubili wavamizi wanaingia ndani ya hifadhi na kujijenga kitu ambacho serikali inapata shida kuwaondoa katika maeneo hayo.
“siyo jambo jema kuanza kuwaondoa Watu kwa njia ya oparesheni wakati viongozi wa vijiji na kata mngeweza kulidhibiti tatizo hilo kwa wakati mambo hayo hayawezi kutokea” alisema
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Nkasi Pankrasi Maliyatabu kwa upande wake alidai kuwa suala la uhifadhi wa mazingira na kulinda chanzo cha maji cha Mfili kinahitaji utashi mkubwa wa kisiasa kutoka kwa viongozi wa kisiasa na kuwa wajitahidi kusema ukweli kwa Wananchi wao juu ya umuhimu wa kuhifadhi chanzo cha maji.
Alisema kuwa suala la uhifadhi wa mazingira halihitaji maneno ya kufurahisha bali ni kueleza ukweli na kila mmoja aweze kujua kwamba kutohifadhi vyema mazingira kutasababisha majanga na kupelekea tatizo la maji na kujikuta katika hari mbaya .
Kaimu mkurugenzi wa bodi ya maji bonde la ziwa Tanganganyika Mhandisi Odemba Cornel amesema kuwa shughuli za kibinadamu kwenye chanzo chochote cha maji ni hatari na ndiyo chanzo kikuu cha kukausha maji kwenye Bwawa na kuwa sasa kila mmoja ana jukumu la kuhakikisha chanzo cha maji hakiingiliwi ili kulinda Bwawa la Mfili na Watu waendelee kupata maji msimu wote.
Washiriki wa mkutano huo wa Wadau kwa upande wao wamedai kuwa mijadala mbalimbali waliyoifanya katika mkutano huo imewajenga na kuwapa ufahamu namna ya kukabiliana na viwezeshi vya uharibifu wa mazingira vinavyoweza kupelekea maji kukauka na kuleta shida kubwa katika jamii.
Rehema Mwakibinga mwakilishi wa mamlaka ya maji mjini Namanyere (NAUWSA) amesema kuwa mkutano huo wa wadau una manufaa makubwa kwao na kuwa kuna matokeo makubwa wanayoyatarajia katika uhifadhi mkubwa wa Bwawa hilo la maji



Comments
Post a Comment