Watendaji wa uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura watakiwa kufanya kazi kwa weredi




Na Israel Mwaisaka, Nkasi

Maafisa Watendaji wa uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura ngazi ya kata wametakiwa kuifanya kazi hiyo kwa weredi mkubwa kama wanavyoelekezwa na kanuni na sheria ili kuweza kufikia lengo kududiwa.

Wito huo umetolewa Leo na Afisa Mwandikishaji wa wilaya Nkasi Ladislaus Mzelela kwenye ufunguzi wa semina ya siku mbili kwa maafisa Watendaji wa uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura ngazi ya kata ambapo amedai kuwa weredi pekee ndiyo utakaowawezesha wao kuweza kufanikisha zoezi Hilo muhimu kwa taifa .




Alisema dhamana waliyopewa kwa kuteuliwa kushika nafasi hiyo ni kubwa na kuwa kuhakikisha zoezi Hilo linafanikiwa ni jukumu lao muhimu kuona kwamba wanavifahamu vikwazo vinavyoweza kufifisha zoezi Hilo na kumtafuta ufumbuzi wa haraka kwa lengo la kuona kuwa kazi hiyo inafanyika kwa kiwango kinachotakiwa .

Pia aliwataka kuzingatia maelekezo ya tume yanayotolewa,huku akiwasisitiza juu ya kuwepo kwa mawakala wa vyama vya siasa kwenye vituo vya kufanikisha wapiga kura ingawa hawatakiwi kuingilia majukumu ya utekelezaji wake

Na amesisitiza suala la ushirikishwaji wa wadau wote wa uchaguzi katika kufanikisha kazi hiyo kwani Kila mmoja anao umuhimu mkubwa Katika kuona zoezi Hilo linafanikiwa kwa kiwango kinachotakiwa.
Watendaji hao wa uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura ngazi ya kata wamepewa mafunzo mbalimbali ikiwemo ya Uraia,ujazaji wa fomu mbalimbali wakati wa zoezi zima la uandikishaji ikiwa ni pamoja na mafunzo ya mfumo wa uandikishaji na vifaa vya BVR Kit.



Zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura linatarajia kuanza Januari 12 na kumalizika Januari 18 ambapo zoezi Hilo inatarajia kufanyika kwa muda wa siku 7.

Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa